Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

SISIS

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Posts
10,892
Reaction score
3,112
Moja ya vitu ambavyo tunavyo baadhi ya wanaume ni kuwachukulia poa wale wanawake wanoonyesha kutupenda kupitiliza, unakuta una mwanamke anakujali mnyeyekevu anakuheshimu alafu unamchukulia poa poa tu wengine tunawanyanyasa tukijua hawana kimbilio sababu ya kuvutiwa na sisi kimapenzi hivyo tunawachukulia kimasihara

My friend siku mwanamke akikuchoka huwa anakuchoka kweli kweli na akigeuza shingo huwa ni mazima kama kashakuvumilia vya kutosha ,akichoka manyanyaso huwa anachoka kweli, ukibahatika kumpata mwanamke mnyeyekevu msikivu anayekujali yaani onyesha kumjalizaidi na kumpenda my friend hawa wanawake wastaharabu wamebaki wachache sana, ukimpata jua umepata dhahabu ndani, wengi walishasombwa na maafuriko kipindi cha mwinyi kwa sasa hawapo wengi wamenaki wachache.

Nayaongea haya sababu kaka yangu kalazwa now siku ya pili presha imepanda, alipata mwanamke mzuri mpolee aliyempenda kupitiliza akamuowa kabisa, yule dada alikuwa anaupendo wa ajabu ukweni , anapendwa ukweni hadi leo, sababu ya tabia zake tu

Ila brother akawa anamchukulia poa anamnyanyasa ,anampiga kesi zikawa zinaletwa hom mara kwa mara , binti akawa anavumilia tu mwaka na miezi sita, sasa juzi bro karudi hom kakuta mkewe kabeba vitu vyake vyote kaondoka kutafutwa kwenye sim anapokea mwanaume anasema muhusika hayupo asisumbuliwe

Kaka kupata hizo habari nusu tumpoteze tumbo la kuhara lilimbana hapo hapo majirani ndio wamemkimbiza hospitali juzi, kufika Bp juu kakata kauli kaaza kuongea jioni ya jana, kachungulia kaburi yani

Saaa kumbe mwanamke alikuwa anampenda kwanini amnyanyase?
 
Ebwana broo umesema neno hapo. Mwenyewe leo yamenikuta aiseh. Huy mwanamke nimekaa naye kweny mahusiano for more than two yrs almost five ila toka juzi naye kanipa kisogo nabembeleza lakn wap. Hapa nahsi moyo unanisuta, nafsi yenyewe inaniuma daaah kweli tukipedwa jaman tupendeke. Nakupenda saan p wangu
 
Ebwana broo umesema neno hapo. Mwenyewe leo yamenikuta aiseh. Huy mwanamke nimekaa naye kweny mahusiano for more than two yrs almost five ila toka juzi naye kanipa kisogo nabembeleza lakn wap. Hapa nahsi moyo unanisuta, nafsi yenyewe inaniuma daaah kweli tukipedwa jaman tupendeke. Nakupenda saan p wangu
Kitu kikiondoka watu ndio huona thamani yake
 
Unasema alimpenda sana mumewe ila kaomdoka na simu anapokea mwanaume mwingine je huyo mwanume amempata siku hiyo hiyo alipoondoka au ulikuwa mpango kando kabla? All in all wanasema usibebe mayai yote kwenye kapu moja! Bro wako alimnyanyasa kama ulivyosema ila hakuwa anapendwa kama unavyohadithia.
 
Back
Top Bottom