Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

Hamna jina naloweza kumpachika brother wako na likampendeza kama jina popoma
 
Mimi nimekuelewa zaidi ya wote. Ulichoandika ni ukweli mtupu. Hii huwa inatokeaga kwa wale wanawake wanaopenda sana kupitiliza, ukimkosea anakuomba yeye samahani, ukimwambia nakuacha atalia nusura ya kufa yaani yuko tayari kufanya jambo lolote ili asikupoteze. Ukitaka waendelee hivyo wapende yaani japo tu mdanganye, ila ukimtesa au akichoka akuacha lazima uumie,

Utajiuliza ni wapi alikohamishia mapenzi Yale na lazima ukonde vile jinga lako limegeuka janja.
 
Kwani watakuwa wameisha watakaokupenda maishanhayo hivyo kunawakati sunchoke basi unaachia
 
Moja ya vitu ambavyo tunavyo baadhi ya wanaume ni kuwachukulia poa wale wanawake wanoonyesha kutupenda kupitiliza, unakuta una mwanamke anakujali mnyeyekevu anakuheshimu alafu unamchukulia poa poa tu wengine tunawanyanyasa tukijua hawana kimbilio sababu ya kuvutiwa na sisi kimapenzi hivyo tunawachukulia kimasihara

My friend siku mwanamke akikuchoka huwa anakuchoka kweli kweli na akigeuza shingo huwa ni mazima kama kashakuvumilia vya kutosha ,akichoka manyanyaso huwa anachoka kweli, ukibahatika kumpata mwanamke mnyeyekevu msikivu anayekujali yaani onyesha kumjalizaidi na kumpenda my friend hawa wanawake wastaharabu wamebaki wachache sana, ukimpata jua umepata dhahabu ndani, wengi walishasombwa na maafuriko kipindi cha mwinyi kwa sasa hawapo wengi wamenaki wachache.

Nayaongea haya sababu kaka yangu kalazwa now siku ya pili presha imepanda, alipata mwanamke mzuri mpolee aliyempenda kupitiliza akamuowa kabisa, yule dada alikuwa anaupendo wa ajabu ukweni , anapendwa ukweni hadi leo, sababu ya tabia zake tu

Ila brother akawa anamchukulia poa anamnyanyasa ,anampiga kesi zikawa zinaletwa hom mara kwa mara , binti akawa anavumilia tu mwaka na miezi sita, sasa juzi bro karudi hom kakuta mkewe kabeba vitu vyake vyote kaondoka kutafutwa kwenye sim anapokea mwanaume anasema muhusika hayupo asisumbuliwe

Kaka kupata hizo habari nusu tumpoteze tumbo la kuhara lilimbana hapo hapo majirani ndio wamemkimbiza hospitali juzi, kufika Bp juu kakata kauli kaaza kuongea jioni ya jana, kachungulia kaburi yani

Saaa kumbe mwanamke alikuwa anampenda kwanini amnyanyase?
Kaka yako kweli bwege...soo it means muda wote huo yeye alikuwa hana pisi kali mbili pembeni ajiliwaze wife akizingua?
 
Huwa kuna upumbafu unatokea na kuanza kuchukulia poa pale mwanamke unapoona matunzo mia toka kwake (I mean "care" ).

Upendo unaona kama unapungua na kumchulia kawaida hivi kisa tumezoea kusumbuliwa sumbuliwa kidogo.

Sasa akichoka acha kabisa. Hata black mamba aliyechokozwa hasira hazifiki wakibadirika.
 
Ndio akome huyo, na wanaume wanaopenda kutesa wanawake Wanaowaheshimu sijui shida huwa nini, maana wanawake wenye tabia njema ndio huteseka kwenye ndoa kuliko mashangingi.
Heheheh kwahio we uko upande gani hapo...shangingi au tabia njema?
 
Ebwana broo umesema neno hapo. Mwenyewe leo yamenikuta aiseh. Huy mwanamke nimekaa naye kweny mahusiano for more than two yrs almost five ila toka juzi naye kanipa kisogo nabembeleza lakn wap. Hapa nahsi moyo unanisuta, nafsi yenyewe inaniuma daaah kweli tukipedwa jaman tupendeke. Nakupenda saan p wangu
Andaa juisi ya ndimu tu kupunguza maumivu ya tumbo.😂😂😂 Tatizo mnawavimbiaga sana huku unajua bila yeye wewe ni kopo tupu!
 
Hakika mkuu. Siku hizi wamejaa wale walioko kwa ajili ya kukukomoa. Akilala anawaza aje na gia gani kukuchomoa. Mapenzi ya siku hizi yamekuwa na hasara nyingi kuliko faida kwa wanaume.
Hahahaha mapenzi ni biashara sikuhizi! Hamna jinsi zaidi ya kuishi nao kwa akili.
Ukipata demu real ukamletea nyodo hakiyamungu nyimbo ya karma utaicheza vibaya mno.
 
Unasema alimpenda sana mumewe ila kaomdoka na simu anapokea mwanaume mwingine je huyo mwanume amempata siku hiyo hiyo alipoondoka au ulikuwa mpango kando kabla? All in all wanasema usibebe mayai yote kwenye kapu moja! Bro wako alimnyanyasa kama ulivyosema ila hakuwa anapendwa kama unavyohadithia.
Hahahahah sasa mwanamke ukimnyanyasa sana sindio anaanza kumegwa nje ambako anapata comfort zone, maana KE akiwa bomba sana jua kila wakati anatongozwa na wanaojua mwanamke mzuri yukoje hawataacha kumsumbua huko nje.

Ila kama mpo in good terms hawapi nafasi hata kidogo. Shida huja pale ambako hamna maelewano mazuri ndani lazma ataachia goli wazi tu hasa akipata mtu wa kumsikiliza na kum comfort nje huko. Sasa kwa vikao vya suluhu ambavyo ni vingi tu vishapita kuhusu bro kuwa msumbufu wacha alazwe tu. Mke hawezi pendwa ukweni kama ana tabia za hovyo! Lazma wangemdiss tu
 
Hahahaha mapenzi ni biashara sikuhizi! Hamna jinsi zaidi ya kuishi nao kwa akili.
Ukipata demu real ukamletea nyodo hakiyamungu nyimbo ya karma utaicheza vibaya mno.
Kwa jinsi manungunyembe yalivyojaa hata akitikea real unaona kama anakuaktia
 
Mimi nimekuelewa zaidi ya wote. Ulichoandika ni ukweli mtupu. Hii huwa inatokeaga kwa wale wanawake wanaopenda sana kupitiliza, ukimkosea anakuomba yeye samahani, ukimwambia nakuacha atalia nusura ya kufa yaani yuko tayari kufanya jambo lolote ili asikupoteze. Ukitaka waendelee hivyo wapende yaani japo tu mdanganye, ila ukimtesa au akichoka akuacha lazima uumie,

Utajiuliza ni wapi alikohamishia mapenzi Yale na lazima ukonde vile jinga lako limegeuka janja.
Umenena
 
Back
Top Bottom