Ukimshitaki Mzigua mkapelekana hadi Mahakamani, uwezekano wa Kushinda kesi ni zero percent

Ukimshitaki Mzigua mkapelekana hadi Mahakamani, uwezekano wa Kushinda kesi ni zero percent

Ramon Abbas

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2021
Posts
1,964
Reaction score
3,913
Nakwambia ukweli,

Uchawi wa Mzigua kwenye kesi ni hatari sana.

Ukishtakiana na Mzigua tegemea kushindwa vibaya sana! Kama wewe si mzigua mwenzie, au hutokei Tanga huko ndio balaa sasa

Kesi ya mzigua utasikia mashahidi wameshindwa kuongea, wamekuwa viziwi ila wakitoka nje ya mahakama wanaongea.

Utasikia File la kesi husika halionekani

Utasikia hakimu akiingia kwenye chumba cha kesi anabanwa na tumbo la kuhara.

Utasikia mashahidi wote wanakukana yani hatari tupu

𝐦𝐛𝐚𝐥𝐢 𝐧𝐚 𝐯𝐢𝐦𝐛𝐰𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐯𝐲𝐚 𝐦𝐚𝐡𝐚𝐤𝐚𝐦𝐚𝐧𝐢,
ukizinguana na mzigua huku uraiani kama kugombea shamba, basi hilo shamba halitokaa liivishd zao lolote lile!!

Mzigua kama alivyo Muha kutoka Kigoma, ana uwezo wa kulima shamba na akaivisha katika eneo ambalo ni makazi ya nyani, na hao nyani wasiguse shamba lake 𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐉𝐢𝐫𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐤𝐚𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐚𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮

𝐌𝐳𝐢𝐠𝐮𝐚, ukimuibia kuku, atakuacha umpike na umle! baada ya hapo atakufanyia kitu hutakaa usahau duniani. Kuku ataanza kuwika tumboni huko mpaka ukaombe msamaha!

Ukiishi Tanga huko uwe makini.

Mfano Handeni huko unaambiwa waganga ni wengi mno, kila baada ya nyumba 2, ya tatu ni ya mganga!

Screenshot_20210921-072906.png
 
Muamini MUNGU shida ya hao jamaa wivu na uvivu nipo Wilaya ya Kilindi nalima nimeshaanzisha miradi kadhaa kwenye shamba langu figisu zao ni nyingi ila wanashangaa navyokomaa, mpaka kutoboa kikubwa usiwape nafasi wakujue kwani watatumia madhaifu yako.
 
Uchawi haupo acha mawazo ya kijinga.

Kwamba mzigua akiua mtu ataroga mahakamani huyo mtu afufuke ili ashinde kesi?

Acha mawazo ya kitaahira.
 
Either wewe mshirikina sana unawazidi au unapiga sala sana, kawaida? Hutoboi hapo Kilindi...
 
Uchawi haupo acha mawazo ya kijinga.

Kwamba mzigua akiua mtu ataroga mahakamani huyo mtu afufuke ili ashinde kesi?

Acha mawazo ya kitaahira.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yaani wew umeelewa hivyo!!
Kweli kuna mtu na binadamu
 
Back
Top Bottom