Endeleeni kulishana matango pori na imani zenu za giza, mwaka 2013 nilienda kununua shamba huko, nilibahatika kupata ekari 50, baada ya kununua nilianza kusikia tetesi kwamba hautokaa ulime, na hata ukilima hautovuna, kwamba utaona mahindi yamebeba lakini ukivuna hupati kitu, au yataliwa na mchwa yote.
Sikuwasikiliza nikajaribu kulima kwanza ekari 10, nikafanikiwa kuvuna nimeendelea hivo na kwa sasa nalima mpka ekari 60, ikitokea mwaka umekuwa mbaya ni kwa sababu ya hali ya hewa na si uchawi.
Ikitokea mchwa umeibuka unadeal nao kwa madawa.
Kujidanganya eti mziguwa hashindwi kesi ni uwezo mdogo wa kufikiri ukichangiwa na makuzi uliokulia yanayoamini ktk waganga wa kienyeji.