Ukimtongoza mwanamke na akakuambia muwe marafiki kwanza ujue hapo amekukataa tayari jiongeze achana naye

Mkuu mimi nina mawazo tofauti na wewe . Kama mwanamke unamtaka kwa uzinzi tu hapo sawa. Lakini kama kwa ajili ya uchumba na ndoa basi urafiki na stage ya kwanza kabisa katika stage tatu za kutengeneza familia.
Urafiki ni muhimu siku za mbeleni pale mnapokuwa kwenye stage ya tatu ya ndoa. Kuna wakati kwenye ndoa kama hamkuwahi kuwa kwenye urafiki Ndoa inakuwa na changamoto fulani fulani.
Mkuu ukibahatika kuoa rafiki yako yaani kuna ahueni kuliko ukaoa tu dada ambaye hamkuwahi kuwa marafiki.
Kwa hivyo ukikutana na dada anakwambia muwe marafiki kwanza basi huyo ana kitu maana hata kama anakupenda atataka pia akujue vizuri wakati wa urafiki.

NB: mimi nilimtaka tukiwa chuoni tuwe marafiki basi tukawa marafiki badaye tukawa wachumba na sasa tuko kwenye ndoa. Kwa kweli ina faida. Tuna miaka mingi ya ndoa lakini tunaweza kuongea kwenye simu hata masaa mawili, atanipa umbea wote aliopata, yaani kuna wakati tunapiga story hadi watoto wanataka kuja chumbani kuuliza tunaongea nini na tunacheka nini. Na ugomvi ukitoa unakuwa ugomvi mkubwa mfano namba ya simu akiitilia shaka yatatikiwa maelezo ya kutosha, ukichelewa kurudi maswali mengi na lugha ya kukera lakini kwa sababh tulikuwa kwanza marafiki tunavumiliana siku zinakwenda.
 
Hii njia yako ilinipiga pini usiku wa manane sitokaa kusahau.

Ila ndiyo uanaume
 
Kwani uhusiano si ndio urafiki wenyewe ulikomaa. Wenye mahusiano ni marafiki.
 
Yaaan hujakubaliwa then unaanza kuita tu pisi ya watu babe,,ujasiri huo wautoa wapi..?
 
Sisi professional players wa zamani, ilikuwa mwanamke akishaniambia tu kwamba tuwe marafiki, huyo tayari nimeshamla; ni swala la muda tu.

Technically, akishakukubali tu kama rafiki tayari anakuwa kakuweka kwenye circle yake. Muda wowote unaweza kumpigia simu, kumuomba muonane n.k, kama ambavyo marafiki wengine wanafanya. Jambo la msingi mno, ni kutokuruhusu akuzoee sana. Weka mipaka.

Hiki kipindi cha urafiki msifie sifie, mnunulie zawadi, mtext mara kwa mara, mtoe outting, mpigie simu n.k. Fanya hivi mfululizo hata kwa wiki 3 (kwa kutegemea na aina ya mwanamke mwenyewe), yani uhakikishe uko akilini mwake muda wote.

Baada ya mwezi au zaidi, ukijiridhisha kwamba kakuzoea (yaani kakuona wewe ni sehemu ya yeye, hata kwa huo anaouita yeye urafiki), wewe badilisha gia angani. Kaa kimya ghafla.

Lazima akuulize kulikoni? Kuwa mnyonge. Lazima aombe muonane. Asipoomba, omba wewe. Ukikutana nae, vunga uko so down. Mwambie wewe kuendelea kuwa karibu naye kama rafiki wa kawaida na siyo mpenzi, kunakuumiza ndani kwa ndani, kwamba umejaribu kujikaza sana sasa umeamua kumwaga manyanga umuache aende, lakini kila ukijaribu kumuacha aende ndio unaumia zaidi (hapa unakuwa umemchanganya zaidi, hatajua unaachana naye au unaendelea na urafiki). Mimi kuna kipindi nilikuwa hadi nafosi machozi yanilengelenge au nakunywa konyagi, kwasababu nyagi ina sifa ya machozi ya karibu [emoji3].

Wallah sheikh, utakuja kunishukuru hapa baadaye. Wanawake wameumbiwa mioyo ya huruma sana. Halafu kwa mwanamke, mapenzi ni jinsi alivyokuzoea na na namna unavyomjali. Ndo mana hapo juu nikasema uhakikishe amekuona wewe ni sehemu ya yeye (hapa namaanisha mazoea).

Nitarudi baadaye [emoji28]
 
Ngoja nianze na hii mbinu
 
Wastage of time! I dont think a rich man can entertain this bullshit! Sorry.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Wastage of time! I dont think a rich man can entertain this bullshit! Sorry.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
Kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha anayotaka
Mbona wako wenye hela wanahonga wanawake wawapendao marange

Achana na hawa wanawake unahitaji sex kwao unapata mda wowote, tunaongelea wale wanawake umewapenda kutoka moyoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…