Ukimuona jamaa yuko na mkeo mjini wanatembea utafanyaje?

Ukimuona jamaa yuko na mkeo mjini wanatembea utafanyaje?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Fikiria uko mjini unakatiza mitaa mara paaap wife na mshkaji halafu wako huru wanagonga mikono na vicheko kibao jamaa humjui wala nini.

Niambie Mkulungwa mwenzangu utafanyaje? Utawapa hai na kuwaacha waendelee na hamsini zao au utawajoin? Niambie Mkulungwa mwenzangu utafanyaje?
 
Namwita wife pembeni kama kuna kitu namuagiza afu namuuliza huyo ni nani? Bila mhusika kusikia

Au nawafuata wote afu namuuliza wife unaelekea wapi saiz

Au nampigia simu kama hawajaniona namuuliza uko wapi wife akinidanganya naanza kuwafuatilia akijibu sahihi namuuliza huyo ni nani

Baada ya hapo natengeneza ratiba nyingine ya ghafla kwa wife ili mradi abadili route na kuelekea nyumbani. Akifika home semina na kipindi cha maswali na majibu kinaanza
 
Namwita wife pembeni kama kuna kitu namuagiza afu namuuliza huyo ni nani? Bila mhusika kusikia

Au nawafuata wote afu namuuliza wife unaelekea wapi saiz,

Au nampigia simu kama hawajaniona namuuliza uko wapi wife akinidanganya naanza kuwafuatilia akijibu sahihi namuuliza huyo ni nani

Baada ya hapo natengeneza ratiba nyingine ya ghafla kwa wife ili mradi abadili route na kuelekea nyumbani. Akifika home semina na kipindi cha maswali na majibu kinaanza
Sikutegemea hii akili kubwa mkulungwa
 
Mmmmh,Kama hawajakuona na jifanye Kama hujawaona endelea na Mishe zako,

Unajua Kuna wanaume wangapi wanalea watoto si wao? Mwanamke anakupigia simu uko mkoani anakwambia Rudi Mara moja Kuna tatizo,

Unafika,tatizo hakuna unaambiwa tu nilikuwa na hamu na wewe,sawa anakuwa sahihi wewe si ndio mumewe?

Nyuma ya pazia kashitukia ujauzito wa mtu mwingine ila ameamua kukutwisha mzigo,
 
Fikiria uko mjini unakatiza mitaa Mara paaap wife na mshkaji halafu wako huruu wanagonga mikono na vicheko kibao jamaa humjui Wala Nini niambie mkulungwa mwenzangu utafanyaje utawapa hai na kuwaacha waendelee na hamsini zao au utawajoin. Niambie mkulungwa mwenzangu utafanyaje.
Niwajoin kwani najua waendako?
 
Naanza kutoa kipigo kwanza tena kipigo chenyewe kinaitwa "bwana yu nasi" then ndo naanza kumsikiliza wakati huo hana meno akiwa anaongea thi thi Kama zote..😅 "thi thi tulikuwa tunaenda thambani kuangalia thamba Kama limethaa.."🤣
 
Back
Top Bottom