UKIMWI bado ni ugonjwa hatari duniani kuliko magonjwa mengine

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Tukiwa tunaadhimisha siku ya Ukimwi duniani leo trh 1/12/ 2024, tusidanganyane, bado ugonjwa huu wa ukimwi ni hatari na tishio zaidi kuliko magonjwa mengine.

Ukimwi ni mateso hadi kifo, chanzo kikuu cha ukimwi ni ngono.

Serikali izuie/ishibiti vyanzo vya maambukizi ya VVU ambavyo ni; madanguro, macasino, vigodoro, n.k

Pole kwa wagonjwa wote wanao endelea kutumia dawa.
 
Tukiwa tunaadhimisha siku ya Ukimwi duniani leo trh 1/12/ 2024, tusidanganyane, bado ugonjwa huu wa ukimwi ni hatari na tishio zaidi kuliko magonjwa mengine.
Ukimwi ni mateso hadi kifo, chanzo kikuu cha ukimwi ni ngono.
Serikali izuie/ishibiti vyamzo vya maambukizi ya VVU ambavyo ni; madanguro, macasino, vigodoro, n.k

Kati (miongoni)ya UKIMWI,malaria,vita na njaa vipangilie kwa takwinu ni kipi kinaongoza kwa kuua.
 
Kwasisi Wanaume wahangaikaji wa maisha kuna msemo wa kukumbushana unasema;

"Furaha yangu ni kurudi nyumbani bila maambukizi"

Tukumbuke Kuna vijana wadogo wanatutegemea kama Baba zao

Hebu tuchukue tahadhali katika mienendo yetu

Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana 💪
 
Kuna magonjwa ya hatari zaidi ya huo ukimwi! Mfano ugonjwa wa kansa na kisukari. Ukimwi ulikuwa hatari miaka ya 1980's na 1990's kabla ya watengenezaji wa huo ugonjwa hawajatuletea haya mashudu yao yanayofubaza makali.

Enzi hizo ukiupata mjini, basi lazima urudishwe kijijini huku ukiwa na uzito wa kilo 2 tu, kwa ajili ya kusubiri siku yako ya kufa.
 
kansa na kisukari ukiwahi matibabu unaweza kudhibiti ugonjwa ukawa fresh tu.

ukimwi ukishaupata hauna namna unaweza kuudhibiti zaidi ya kunywa dawa maisha yako yote tena ni kila siku. ukiacha dawa vidudu vinakamata koromeo lako au ubongo apo lazima ukate moto.

ukimwi hutokana na ngono(>95%) ni ugonjwa wa kuaibisha sana ndomaana ni nadra mhusika kujiweka wazi wkt wa kuumwa na hata kwenye umauti wengi husingizia kansa presha na kisukari. iyo inamaana sio ishu mtu kuwa na kansa presha au kisukari. tuombe tu mungu aingilie kati ukimwi upate tiba maana watu weusi kwa tabia zetu za kupenda ngono tutaisha wote.
 
Tukiwa tunaadhimisha siku ya Ukimwi duniani leo trh 1/12/ 2024, tusidanganyane, bado ugonjwa huu wa ukimwi ni hatari na tishio zaidi kuliko magonjwa mengine.
Ukimwi ni mateso hadi kifo, chanzo kikuu cha ukimwi ni ngono.
Serikali izuie/ishibiti vyamzo vya maambukizi ya VVU ambavyo ni; madanguro, macasino, vigodoro, n.k
Pole kwa wagonjwa wote wanao endelea kutumia dawa.
Na mwenge nao unachangia pale unapoenda kulazwa nao upigwe marufuku
 
Tukiwa tunaadhimisha siku ya Ukimwi duniani leo trh 1/12/ 2024, tusidanganyane, bado ugonjwa huu wa ukimwi ni hatari na tishio zaidi kuliko magonjwa mengine.
Ukimwi ni mateso hadi kifo, chanzo kikuu cha ukimwi ni ngono.
Serikali izuie/ishibiti vyamzo vya maambukizi ya VVU ambavyo ni; madanguro, macasino, vigodoro, n.k
Pole kwa wagonjwa wote wanao endelea kutumia dawa.
 
Kuna magonjwa ya hatari zaidi ya huo ukimwi! Mfano ugonjwa wa kansa na kisukari. Ukimwi ulikuwa hatari miaka ya 1980's na 1990's kabla ya watengenezaji wa huo ugonjwa hawajatuletea haya mashudu yao yanayofubaza makali.

Enzi hizo ukiupata mjini, basi lazima urudishwe kijijini huku ukiwa na uzito wa kilo 2 tu, kwa ajili ya kusubiri siku yako ya kufa.
Kwani ukiwa na UKIMWI huwezi kupata na kansa pia ?
 
UKIMWI ikiwa ni tatizo la jamii chanzo chake kikubwa ni umaskini, na kama tunavyojua tatizo la jamii likifungamana na umaskin haliondoki mpaka umaskin uondoke. Ukiangalia takwim za wagonjwa wake wanawake wa umri fulani ndo wanaomgoza, vijana wa umri fulani kiujumla. Umri huo ukiuangalia vizur utaona wemgi ni dependents pamoja na unri huo kuwataka wawe economic actives

Miradi ya kuinua watu kiuchumi ina madhara chanya katika kupunguza rate ya ongezeko la ukimwi kufikia 95-95-95
 
Back
Top Bottom