UKIMWI bado ni ugonjwa hatari duniani kuliko magonjwa mengine

UKIMWI bado ni ugonjwa hatari duniani kuliko magonjwa mengine

Kwasisi Wanaume wahangaikaji wa maisha kuna msemo wa kukumbushana unasema;

"Furaha yangu ni kurudi nyumbani bila maambukizi"

Tukumbuke Kuna vijana wadogo wanatutegemea kama Baba zao

Hebu tuchukue tahadhali katika mienendo yetu

Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana 💪

Nimeependa hiyo moto.
"Furaha yangu ni kurudi nyumbani bila maambukizi"
Tuendelee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunusurika miaka ya 80 mwishoni mpaka 90 mwishoni. Hali ilikuwa mbaya. Hata ukiwa baunsa vp, ukiupata lazima uondoke na kilo 2.

Gen Z haya yote hawayajui, ndiyo maana hawatulii.
 
Hakika ni hatari Mkuu

Ukimwi wa zamani ungeweza kumtambua mtu Kwa macho Kwa namna alivyoisha, huu wa nyakati hizi unakutana na binti kisu kweli, kumbe ndiyo anao.

All in all, tahadhali muhimu kuchukuliwa
 
Siku hizi ukimwi kama mafua tu! Umeona watu na afya zao ila wana VVU. Dawa ya pekee ni kukubaliana na hiyo hali na unachapa maisha kama kawa. Sema tu adhabu ni dawa za kila siku.

Ni kweli kabisa. Dawa za kila siku ni changamoto. Ila wataalam wana develop m'badala ambao mtj mwenye VVU atakuwa akichoma mara 2 kwa mwaka.

Pamoja na maendeleo haya, bara letu bado lina mchango mdogo San katika mapambano haya. Bado hatujasimama wenyewe kwenye kutengeneza madawa na tafiti. Bado ni tegemezi. Hivyo sera za wanaotusaidia zikibadilika na kuwa siyo upande wetu. Inaweza ikala kwetu. Hivyo elimu iendelee kutolewa kuhusu VVU. Maana gen z ambao ni sexually active group wana uelewa mdogo sana kuhusu ukimwi. Na hawaja wahi ona yule mgonjwa wa ukimwi wa miaka ya 90 kati kati.
 
Kwasisi Wanaume wahangaikaji wa maisha kuna msemo wa kukumbushana unasema;

"Furaha yangu ni kurudi nyumbani bila maambukizi"

Tukumbuke Kuna vijana wadogo wanatutegemea kama Baba zao

Hebu tuchukue tahadhali katika mienendo yetu

Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana 💪
Ameen ameen.

Ukimwi upo. ....tuzidi kuchukua tahadhari
 
Ameen ameen.

Ukimwi upo. ....tuzidi kuchukua tahadhari
Hakika Mkuu

Kuna watu wanatutegemea Kwa Kila kitu, na ndiyo kwanza unakuta wapo class II ama VII

Vyema tuendelee kuchukua tahadhali

Jay Mo Kuna sehemu aliwahi kuimba "...hakuna demu wa kwenda naye nyama Kwa nyama...."

Wimbo uliitwa Jirushe, akiwa na Ferouz
 
Siku hizi ukimwi kama mafua tu! Umeona watu na afya zao ila wana VVU. Dawa ya pekee ni kukubaliana na hiyo hali na unachapa maisha kama kawa. Sema tu adhabu ni dawa za kila siku.
Shida kubwa ni hapo kwenye kukubaliana na hiyo hali,wengi hapo ndio mtihani,kifupi tuache uzinzi,hata hao wanaotumia dawa sio rahisi hivyo unavyofikiri,ni kupanda na kushuka,leo mzima kesho mgonjwa...
 
Pamoja na maendeleo haya, bara letu bado lina mchango mdogo San katika mapambano haya. Bado hatujasimama wenyewe kwenye kutengeneza madawa na tafiti.
unaongelea mambo ya mbali sana mkuu, mtu mweusi na mambo ya utafiti wapi na wapi? sisi mchango wetu unatakiwa uwe ni wa kufanya ngono salama maana hatuwezi kuacha ngono
 
Watu wa maofisini muwe makini na wadada/wakaka wapya ndani ya ofisi zenu maana hamjui background zao
 
Ni mpaka dawa itakapogundulika si vinginevyo!
Hata serikali ipige marufuku Madanguro,Cassino,nk
haiwezi kusaidia!
Siku hizi hata mabarabarani,uchochoroni,vichakani,majumba ambayo hayajaisha! Magetoni,nk ni uchafu mtupu!
 
Kuna magonjwa ya hatari zaidi ya huo ukimwi! Mfano ugonjwa wa kansa na kisukari. Ukimwi ulikuwa hatari miaka ya 1980's na 1990's kabla ya watengenezaji wa huo ugonjwa hawajatuletea haya mashudu yao yanayofubaza makali.

Enzi hizo ukiupata mjini, basi lazima urudishwe kijijini huku ukiwa na uzito wa kilo 2 tu, kwa ajili ya kusubiri siku yako ya kufa.
Sasa kwa taarifa yako ukiwa na huo Ukimwi kupata Kansa na Kisukari ni rahisi zaidi

kuliko mtu asiyokuwa nao.
 
Kuna magonjwa ya hatari zaidi ya huo ukimwi! Mfano ugonjwa wa kansa na kisukari. Ukimwi ulikuwa hatari miaka ya 1980's na 1990's kabla ya watengenezaji wa huo ugonjwa hawajatuletea haya mashudu yao yanayofubaza makali.

Enzi hizo ukiupata mjini, basi lazima urudishwe kijijini huku ukiwa na uzito wa kilo 2 tu, kwa ajili ya kusubiri siku yako ya kufa.
Aisee hizo enzi ilikuwa hatari Sana🤔
 
Back
Top Bottom