Ukimwi unaniuwa kwa haraka jamani

mh! yaani hata hodi hakuna jameni...unaingia tu na kuja na stori zako za kugegedana kavukavu! lkn pole!
 
Kavu kavu raha jamani, sijui tufanyeje. Hasa ukizingatia unakutana na katineja...
 

Mkuu sijakuelewa vizuri hapo pekundu.Ungefafanua vizuri kwa faida ya wengi.
 
Yaani mwezi mmoja tu uanze kupata magonjwa nyemelezi?!!.
Wewe utakua umepanick.

Hofu ni ugonjwa mbaya sana,ndugu yangu tuliza akili yako.Uliposikia mdada ni mwathirika ulipanic.Ndicho kinachokusumbua nenda angaza watakupa ushauri mzuri sana.
 
Mkuu sijakuelewa vizuri hapo pekundu.Ungefafanua vizuri kwa faida ya wengi.



Mtu mwenye ukimwi/AIDS ana dalili zinazoonekana dhahiri ndizo kazitaja hapo juu. Kwa hali ya kawaida dalili hizo husababishwa na HIV. Sasa kuna baadhi ya wagonjwa wana dalili zote hizo lakini wanapopimwa hawakutwi na HIV ... Soma post zangu nyuma nimesama kuna uwezekano.. EMOTIONAL PARASITES ...

Utaelewa zaidi uki google " AIDS WITHOUT HIV" ukasoma kwa makini...
 
Pole ana ndugu yangu, unajua si vizuri kuchanganyikiwa hali hujahakikisha kwamba u mgonjwa au umeathirika, nachoamini mimi ni kwamba, kujua kwamba u mzima au mgonjwa ni tiba tosha ndugu yangu .fanyavipimo uweze jua kisha ujitunze.
 

Mkuu asante kwa msaada wako, naomba kujua pia ghalama zake maana nilifika hapa Singida rufaa wakasema hakuna zaidi ya hizo za miezi 3. Nikijua ghalama zake naweza kujipanga na kuja Dar maana ndipo karibu kutoka hapa Singida. Asante tena
 

Asante sana mkuu kwa kuchukua muda wako na kunishauri mambo mengi muhimu. Mkuu tangu nijue hali ya yule kimwana sasa ni wiki ya 6 na siku 5 yaani zimepita siku 40. Sio rahisi sana kufika hapa maana niko vibaya emmotionally na sioni tumaini japo nadhani nikijua hali ya afya yangu naweza jua nini chakufanya.

nikijua nimeathirika inakuwa hakuna namna tena nitakubali matokeo na itanilazimu kuishi maisha ya virusi. Tafadhali iwapo unafanya kazi katika vituo vyenye huduma hii nisaidie kipimo mkuu nijifahamu.
 
Hapana ndugu.
Hii ni post yake ya kwanza,anaonekana amejiunga leo tu. Tatizo ninaloona kwake ni kwamba,mbona amepost kisha amejiweka pembeni kimya? Hakuna response tena.

sijaamua kukaa pembeni mkuu tatizo sina computer ya kuwa online muda wote. Nisaidie na endelea kufanya hivyo
 
Hapana ndugu.
Hii ni post yake ya kwanza,anaonekana amejiunga leo tu. Tatizo ninaloona kwake ni kwamba,mbona amepost kisha amejiweka pembeni kimya? Hakuna response tena.
wengine hufungua id mpya,maybe ni mtu mzoefu humu jf.pole kijana.wasiwasi pekee unaweza ukajihisi una dalili zote kumbe ni wasiwasi tu huo.ugonjwa uusikie tu kwa mwenzako,maana hiyo presha yake huwa si ndogo.na mara nyengine mwengine anajiamini kabisa kuwa huu ugonjwa hatoupata,na anawanyooshea wengine vidole.bila ya kutegemea unapima na kupata majibu kuwa umeathirika.kibaya zaidi ni kudeal na watu wako wa karibu,kuna watakaokusema,kuna watakaokuonea huruma.mradi kila mtu na lake
 
Poleni sana. Mwamini sana Mungu hakuna lisiliwezekana kwa Mungu.
 

Asante sana kiongozi kwa maneno ya faraja kubwa sana maishani mwangu, maana hata aliyekuwa mpenzi wangu baada ya kumwambia hii kitu aliniacha gheto na hajawahi kunipigia simu tena. Lakini wewe unenifariji kwa dhati ya moyo wako mkuu wangu.

nimepata nguvu mpya ya kuishi kwa miaka mingine mingi tuu hata zaidi ya 50 za ulaya endapo nitakuwa nimeoza na virusi.

Lakini pia Mungu akinisaaidia kuwa salama UMAYA sasa itakuwa basi. Nitaanza maisha ya uaminifu sana na kujenga familia yangu , lakini pia nikiwa nao nitakubali matokeo na niutunza ndani yangu pekee maana sio vyema sana kuwaingiza wengine kwenye janga hili. Maana watakuwa hawakutendewa haki nami.
Asante tena Mkuu maana kama wangenipa PEP pia yamkini ningekuwa salama maana nilipima baada ya saa moja tangu nitoke mtamboni
 

We unaujua ukimwi au....jishauwe tu na mahekaya ya abunuwasi haya unayoandika humu kuna siku utaupata kweli jasho litakutoka
 
Mhhhh....uko kwenye window period, subir baada ya 3 months ukafanye full blood picture 😉
 

Surua ndo unafeel aje?
 

Mkuu kwani hiyo PEP unapewa ARV utumie? Nataka nijue tu mkuu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…