Ukimwi unaniuwa kwa haraka jamani

Ukimwi unaniuwa kwa haraka jamani

Acha uoga hata malaria iko namna hii,
Unaweza kukuta una typhod ama tb,
Ukificha unahatarisha maisha,
Ni bora kusubiria,
Ujue kama umeambukizwa eeeeeh!
 
hivi huyu sio yule alikuja na stori kafiwa na mkewe ili aonewe huruma na wanawake wa humu?mie hizi drama za humu siziwezo...lol:yo:

Hapana mkuu huyu ni Mwakambaya2013 ana amejiunga leo JF. Unless kama amekuja kivingine. Ni wiki 6 tu tangu afanye ngono isiyo salama so anaomba ushauri ila nashangaa kuna watu wanamnyanyapaa sana. So sad.
 
We unaumwa zaidi saikplojia... acha uoga. Zaidi ya 55% ya wanaume wanaofanya mapenz na wanawake waathirika kwa mara moja hawapati maambukizi. Hii ina maana kuwa una 55% probability ya kuwa hujaathirika. Pili, hata kama umeathirika, una zaidi ya miaka 5 kabla hujaanza kupata magonjwa nyemelezi (CD4 kushuka sana). Tatu, hata baada ya CD4 kushuka sana, una zaidi ya miaka 15 ya kuwa na afya njema kwa kutumia ARVs.

Kwa hiyo, Kwanza 55% kuwa hujaathirika, pili, miaka 5 kabla hujaugua, tatu miaka 15 au zaidi ya kuishi na afya kwa ARV..
miaka 5+15=20... hiyo ni minimum... ina maana hata kama kwa bahati mbaya uliambukizwa, una zaidi ya miaka 20 ya kuishi. Hivi hadi miaka 20 ijayo, tiba ya HIV itakuwa haijapatikana kwa kweli? Mi nadhani itakuwa imepatikana...

So, ondoa hofu mdogo wangu... miaka 20 inakutosha kutimiza ndoto zako zote za maisha. By the way unaweza shangaa hata kama usingeathirika na HIV, ndani ya hiyo miaka 20 (au zaidi, maana tafiti zinazidi kugundua dawa imara kila zaidi kila siku), ungekufa labda kwa moyo, cancer au ajali... so kifo kipo tu hata usingeambukizwa...

In addition, kwa nchi zilizoendelea kama ulaya wanatumia 3rd generation ya HIV, inayompa mtu uhakika wa kuishi zaidi ya miaka 40 baada ya kuathirika. Kwa Tanzania kwa sasa tunatumia ARV duni kwa sababu ya ukata wa serikali. Hata hivyo ARV hizo bora zimeanza kushuka bei huko duniani, na bila shaka ndani ya miaka michache, Tz itaanza kuzitumia, na utahakikishiwa kuishi hadi miaka 50 kutoka sasa... Sasa mdogo wangu una miaka mingapi sasa hivi... kama utaishi miaka 50 ijayo, kuna haja ya wewe kuwa na wasiwasi?

Nikuambie kitu... kama unasoma, au unafanya kazi, basi fanya bidii ili baadae uwe na ela ya kutosha kula na kugharamia dawa. Pia kama unasoma, soma kwa bidii ili baadae usilazimike kufanya kazi ngumu na hatarishi, zitakazoyaweka maisha yako hatarini...

Sawa e? Dont worry... wengi unaowaona humu, au huko uliko wanacheka, wanaishi kwa furaha ni waathirika, but hawana wasiwasi na wanaishi maisha mazuri na yenye afya zaidi ya maelfu ya wengine ambao hawajaathirika...

Lastly... Why worry if you can pray? Mungu wako hawezi kukuadhibu na kukutelekeza kwa dhambi moja bana... kula maisha... nothing has changed in you

By the way we ni mzima... hujaathirika...

Well done Dr. Tuko. Kwa hakika nakushukuru mno kwa ushauri huu. Nimecopy na kuhifadhi maana najua kwa maisha yetu ni lazima tuwatie watu faraja kwa kuaeleza kuwa kuna maisha baada ya kupata VVU. Wapenzi wana JF suala la HIV and AIDS si la kubeza hata kidogo. Usipoukwaa wewe ataukwaa rafiki, ndugu yako wa damu, wazazi, watoto wako au mtu mwingine anayekuhusu sana. Kwa mantiki hii hakuna sababu ya kumrushia au kumnyooshea kidole mleta mada Mwakambaya2013.
 
ninmwezi mmoja tu tambu ni fanye mapenzi na dada ambaye baada kumfanya tulienda maabara kupima maana nilimuona anavutia sana na alikuwa na umri wa miaka 19 tu hivyo nikaamini atakuwa mzima. Baada ya kumfaidi nikajenga hoja ya kujua afya zetu na tulivyopima sikuamini matokeo binti alikutwa na UKIMWI na hakuwa na wasiwasi kabisa akaanza kunipa pole.

Naomba msaada wandugu kama kunaaina ya kipimo ambacho naweza kufanya nikawa na uhakika wa afya yangu maana mala tumbo, kichwa, usingizi saa 8 unakatika, kichefuchefu, mafua na kikohozi, mwili kuwasha. hayo ni machache tu kwa dalili na magonjwa niliyonayo.

haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.

Usiwe na hofu!! Wewe ni mzima kabisa!! Amini hivyo na ukipima utakuwa salama. Ila pia kama si salama umeshapata ushauri hapa wa jinsi ya kuishi. Uwe na mawasiliano ya karibu na watu wote hapa (IDs) waliokuwa positive kwa shida yako just incase mambo yakiwa mabaya. Wako akina Tuko na wenzake, please copy hiyo post yake na itakusaidia kila siku uwe unaisoma pindi utakapokuta hali si njema. Ukiwa na HIV ni bora kuliko kuambiwa una cancer ya koo au tumboni au mapafu ambayo kwa watu wengi maximum wanaishi nayo kwa miaka mitatu tu!! hasa kama huna hela nyingi za tiba na virutubisho. Kwa HIV unaishi hata miaka 10 bila signs za AIDS (kushuka kwa CD4 na kugua magonjwa nyemelezi) na ukianza kutumia ARV kwa kufuata taratibu zake basi unahesabu miaka kibao ya kuishi. Kuna maisha tena marefu sana baada ya kupata HIV! Tena ukifahamu mapema itakusaidia kuanza kula hata diet ya nzuri na kupunguza baadhi ya mambo kulingana na ushauri wa vituo vyao. Huwa napima mara kwa mara kwa kuwa ukishakuwa na mahusiono yawe katika ndoa ni vema ujue afya yako maana hujui mwenzio anafanya nini. Kujua mapema kutasaidia kujiweka fresh kuliko kuja kushtukizia magonjwa nyemelezi tena kwa hofu kubwa kiasi kwamba CD4 zinashuka kwa kasi zaidi kwa sababu ya shock. So nakushauri kapime baada ya miezi hiyo 3 (75% majibu kuwa sahihi) na miezi 3 baaday (6 months in total) ambayo ni 95% majibu kuwa sahihi. Do not worry HIV haiu kama Cancer!! We love you na ukipata majibu share nasi hapa. All the best na tafadhali ID yako ya Mwakambaya2013 inakunyanyapaa pia. Omba Mods wakubadilishie jina kwa kuwa PM invisible au mwingineyo na itabadilika fasta. Asante na uwe na amani.
 
asante mkuu lakini kuna aina ya kipimo kiitwacho PCR kuna member kashauri je nacho sio cha uhakika sana?
 
Namshukuru mkuu Ngahekapahi hapo juu kailezea vizuri sana...

Niliwahi kumtania dk mmoja kuwa kama PEP inasaidi, then mtu ukisex labda katika mazingira ambayo hukujikinga (hasa ulevi), je unaweza kwenda hospitalini kesho yake ukapewa... akacheka, akasema ukipewa itakusaidia, but sio rahisi kwa madaktari wa kibongo kukuelewa...

Nadhani kuna haja ARV zianze kuuzwa pharmacy kama aspirin...
anyways siafiki ARVS kuuzwa madukani kama asprin as zikitumiwa abuseful zaweza kuleta madhara makubwa sana, matumizi ya PEP husaidia sana kuzuia maambukizi mapya.kinachonishangaza ni kwanini hizi zisitumiwe ama wanahofia watu ndo watakuwa wabaya zaidi??ila kwa watu wa maabara wao hutumia sana hizi dawa kujikinga na maambukizi.
 
Elisa ni kipimo cha uhakika ila unaweza ukajijuapia.

Kama baada ya ngono ulipata homa kama ya flu, au mwili ukawa kama una surua vile, uwezekano kama umepata maambukizi ni mkubwa.

lakini wewe, watu wanaimba nyimbo, michezo ya kuigiza, filamu matangazo kila aina, documentaries zote unaona ni bure?
Huna huruma kabisa kwa watu wanaokupenda.
Sikunyanyapai lakini hustahili moral support kwani haionyeshi kama ni bahati mbaya bali ulifanya makusudi ukijua fika hatari ya ngono zembe.
Hata hivyo I hope uko salama, nisingependa mtu yeyote apate maambukizi. I have been affected so many times by AIDS in the FAMILY

Homa ya flu??na mwili kama ulipata surua baada ya ngono??how embu fafanua.me ndo nasikia kwa mara ya 1 hili.so ina maana baada tu ya ngono ukipata homa ya flu na au ukipata vipele mwili mzima maanake surua ni vipele vidogo vidogo basi mtu ahesabu ameathirika??du we mdau fafanua hapa usichanganye watu
 
you need counseling. go to your nearest health centre and explain urself, but jus to encourage u. among 100 men who have unsafe sex wid HIV positive women, only 5 to 10 of dem are infected.nb; kuna kipimo kinaitwa PCR kinapima viral RNA and viral PROTEIN ni kizuri zaidi kuliko hizo antibody test bt its very expensive kwa referal hospital only. pole sana bro and next tym usisahau kuvaa BUTI.
 
Muhimbili kuna kitengo maalum cha kupima ukimwai kiko karibu na wodi ya magojwa ya akili ni gorofa la rangi ya cream na wana kipimo cha elisa na utapata ushauri kutoka kwa wataalamu jinsi ya kujizuia usipate maabukizi.nakutakia kila la kheri.
 
pole mdogo wangu... beauty is deception!
hayo magonjwa uliyonayo yanatokana na hofu kuwa maybe umeukwaa! ondokana na hofu hiyo kwanza!
 
Ndg hakuna ambukzo la wk 6 zen dall zkawa nyng kiasi hcho, just punguza kuwaza na jtahd kusahau. tafta kwanza uhakka, je km huna ambukzo.
 
haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.

Dugu
Ukila asali lazima ujilambe!
Una haraka ya nini kujua vipimo mapema?
Umeambiwa usubiri miezi mitatu, miezi mitatu sio mingi. Fata ushauri wa Zuma; kimbilia bafuni na uwe unaoga mara 6 kwa siku.

Kama katika kipindi hicho cha miezi mitatu utapata mapepo ya kulamba tena asali , rudi kwa huyo dada wa miaka 19, usije ukawapa wengine shauku uliyonayo wewe sasa ya kutaka kujua hali za afya zao baada ya kukupatia asali.

Kama baada ya miezi mitatu utaambiwa, umechuma "chungu/tamu" ya kulamba asali kiovyo ovyo, basi uende ukafunge ndoa na mrembo wako wa miaka 19 ili muwe mnapeana pole, huku mnakula asali yenu pamoja hadi pale mtakaporudisha number.

Wasiwasi ni maradhi tosha ,kwa hiyo punguza hofu..jiandae kisaikolojia kupokea matokeo ya uchunguzi wa afya yako baada ya miezi mitatu.....Mkulu angekwambia,"usiwe na kiherehere"

Mshahara wa dhambi........

Na ujanadume ni pamoja na kujikaza baada ya kupata "mtihani mgumu"...usiwe kama vijana waliofanya mtihani wa kidato cha nne.
 
Sitaki kuamoni kuwa ndani ya wiki sita magonjwa nyemeleziyameanza kwa kasi,kama ni hivyo si bure mwili wako umedhoofika kabisa
 
Dugu
Ukila asali lazima ujilambe!
Una haraka ya nini kujua vipimo mapema?

Mshahara wa dhambi........]

Sina haraka sana mkuu ya kutaka kujua hali yangu, lakini natamani kujifahamu maana kulikuwa na kengine kazuri zaidi sana ya yule sitaki kukaua iwapo nitakuwa na tatizo. Kamekuwa kakitamani kuja Home mala nyingi nikape mambo lakini naogopa kukaambukiza. Nakama nilivyosema hapa Singida rufaa hakuna kipimo hicho.
 
Dah,huu ugonjwa jamani umekaa pabaya sana,nimekuwa nikijiuliza hivi siku chanjo ya HIV au dawa ya kutibu HIV itakapopatikana uzinzi utaongezeka kwa kiwango gani,maana kuna watu wameamua kuacha uzinzi only because they afraiding of the disease,msije pia mkajisifia kuwa mke/mume wangu sio malaya kabisa jua kuwa siku chanjo au dawa ikipatikana ndio utajua tabia halisi ya mume/mke wako concerning uzinzi.
 
Na wewe kwa umbea umezidi jamani hi heading umeandika kwa uzito mie nikajua upo kitandani hujiwezi.Basi nilikuja na mambo mengi mazuri ya kukufari ila kwa hiii story yako nayaifadhi sintokwambia.Kw aleo nakupa pole tu na usubilie miezi mitatu ndo ukuje hapa kutwambia majibu tujue kama ni + au -.
 
ninmwezi mmoja tu tambu ni fanye mapenzi na dada ambaye baada kumfanya tulienda maabara kupima maana nilimuona anavutia sana na alikuwa na umri wa miaka 19 tu hivyo nikaamini atakuwa mzima. Baada ya kumfaidi nikajenga hoja ya kujua afya zetu na tulivyopima sikuamini matokeo binti alikutwa na UKIMWI na hakuwa na wasiwasi kabisa akaanza kunipa pole.

Naomba msaada wandugu kama kunaaina ya kipimo ambacho naweza kufanya nikawa na uhakika wa afya yangu maana mala tumbo, kichwa, usingizi saa 8 unakatika, kichefuchefu, mafua na kikohozi, mwili kuwasha. hayo ni machache tu kwa dalili na magonjwa niliyonayo.

haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.

HOFU inaua! ukileta mchezo utakufa kwa hofu na si kwa ukimwi. Tuliza akili yako uwe tayari kwa lolote wewe hutakuwa wa kwanza kuugua hadi kufa kwa ukimwi. Huna haja ya kujiweka roho juu, vuta subira na muda wa kupima ukifika utaenda kupima tena; sioni sababu ya kujiweka roho juuu mapema nanmna hii. tulia
 
Back
Top Bottom