GreenMiles J
New Member
- Aug 6, 2011
- 2
- 5
Karibu miezi mitatu sasa imepita tangu niwasilishe maombi ya pasipoti, lakini hadi leo (Machi 2026) sijapatiwa huduma hiyo kutoka Idara ya Uhamiaji Tanzania. Kila ninapofuatilia naambiwa kuwa ‘mfumo unaboreshwa.’
Swali ni: Maboresho haya yana mwisho lini, na kwa nini hakuna taarifa rasmi, ya wazi na ya kuwajibika kwa umma kuhusu hali hii? Wanajua tunachopitia hadi kufikia hatua ya kulalamikia Mtandaoni kama hivi?
Si mimi peke yangu ninayepitia changamoto hii; malalamiko ni mengi pia mtandaoni na hata kwenye kurasa rasmi za Uhamiaji. Je, mamlaka husika zinafahamu madhara ya ucheleweshaji huu kwa wananchi wenye safari, matibabu, masomo, kazi, na majukumu mengine ya msingi? Je, wanaona kuwa ukimya wao ni jibu tosha kwa watu wanaohitaji huduma kwa wakati?
Wananchi wanastahili si tu huduma, bali huduma yenye uwazi, mawasiliano ya heshima, na majibu yenye matumaini. Kama huduma zimekwama, semeni wazi. Kama kuna changamoto, elezeni. Kama kuna muda wa kurejea kwa huduma, tawajulisheni watu.
Kimya cha muda mrefu mbele ya kilio cha wananchi wenye uchungu hakijengi imani kinazidi kuumiza na kukatisha tamaa.
Pia soma:
~ KERO - Idara ya Uhamiaji Arusha unaomba Pasipoti leo unaambiwa usubiri miezi mitano au 6, inaumiza sana hii!
~ Uhamiaji wanakera kwa kuchelewa kutoa hati za kusafiria
~ Maafisa na Askari wa Uhamiaji tunateseka kwa uhamisho bila malipo
~ Kuna harufu ya rushwa Idara ya Uhamiaji kutumika kuhuisha vibali kwa raia wa China waliomaliza muda wa kuwepo nchini
~ Baadhi ya Maafisa wa Uhamiaji Wilaya ya Muleba wanatumia 'Road Barrier' kula rushwa