Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Mada Fikirishi
Katiba yetu inaongelea kifo cha Rais akiwa madarakani lakini haiongelei Mgombea Urais ambaye tayari ni Rais akifa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Natoa mfano ili uelewe kwa urahisi kwamba JPM angekufa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu Katiba haisemi kitu gani kifanyike zaidi tu ya kusema nafasi ya Rais itachukuliwa na Makamu wa Rais. Sasa yafuatayo hayana majibu ya Katiba:-
1. Je, kama Mgeombea Urais akifa kwenye kampeni za uchaguzi nafasi yake itajazwaje?
2. Je, Makamu wa Rais anayerithi kiti cha Rais ndiye atakuwa Mgombea nafasi ya Urais?
3. Je, atateuliwa mwingine na chama kujaza nafasi ya Mgombea Urais? Au atajaza nafasi ya Makamu wa Rais kwa kuwa Makamu wa Rais aliyekuwepo tayari amerithi kiti cha Rais na kuwa Rais?
4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?
5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?
6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?
7. Japokuwa iko wenye Katiba kuhusu kifo cha Rais akiwa madarakani lakini kama taifa hatukujiandaa na kifo cha Rais akiwa madarakani, ni vivyo hivyo kumbe kwamba hata sasa kama taifa hatujajiandaa na kifo cha Rais ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais; kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Kipi kifanyike? Au tuige Katiba ya Urusi ambayo Rais anaweza kuondoka Ikulu na akawa Waziri Mkuu na kurudi kuwa tena Rais Ikulu?