Mkuu, naomba nikusaidie maana unachanganya mambo mawili. Mambo unayochanganya moja linahusu kumpata Rais endapo Rais amefariki, pili ni kumpata mgombea wa kiti cha Rais endapo mgombea amefariki wakati wa Kampeni.
Ikiwa Rais mfano Magufuri angefariki wakati wa Kampeni ( wakati wa kugombea muhala wake wa pili) ,yafuatayo yangefanyika. Kwa kuwa kiti cha Rais kingebaki wazi utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais ungefanyika yahani makamu wa Rais angeapishwa kuwa Rais wa nchi.
Pili,kwa kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kingekuwa kimepoteza mgombea sharia ya uchaguzi inataka chama kilichopoteza mgombea kujaza ( kuteua) mgombea ndani ya wiki mbili,alafu mchakato wa uchaguzi ungeendelea.
Kutokana na utaratibu huo, ingebaki utashi wa CCM kuamua kama Samia S.Hassan ateuliwe kuwa mgombea au wateue mwingine. Hivyo katiba katika hilo haijanyamaza, tatizo ni wewe na watu wa aina yako kutokutofautisha mambo ya serikali na yale ya CCM kama chama.
Baada ya ufafanuzi huu wa chumla nitakuwa najibu hoja zako mojamoja.
Sent from my TECNO L9 Plus using
JamiiForums mobile app