Ukimya wa Katiba ya JMT Kuhusu Kifo cha Mgombea Urais

Yani jamaa.hawaamini kuwa kuna kifo na kuna Mungu
Wanataka kumdhuru hangaya ili wawe na amani
Kwa Tabia zao za mauaji tunavishauri vyombo vya Usalama hususani TISS kuhakikisha wanazidisha ulinzi na intelligensia ya Rais
 
1. Je, kama Mgeombea Urais akifa kwenye kampeni za uchaguzi nafasi yake itajazwaje?

2. Je, Makamu wa Rais anayerithi kiti cha Rais ndiye atakuwa Mgombea nafasi ya Urais?
Mbona haya ni rahisi Sana.
Katiba yetu inasema "mtu atakoma kuwa rais siku ambayo rais mwingine atakpokula kiapo.

Sasa endapo JPM angekufa wakati wa kampeni 2020, Samia angechukua nafasi yake. Chama chake kingemtafuta VP kama walichofanya JPM alipokufa kweli.

Kuhusu nani angekuwa mgombea. Kampeni husitishwa kwa miezi mitatu. Halafu chama chake kingefanya mchakato wa kumpata mgombea kwa mujibu wa utaratibu wa chama chake
 
Hamna mada fikirishi hapa ni uvivu tu wenu wa kutafuta maarifa....mgombea urais akifariki kwenye kampeni zoezi zima linaitishwa upya Chama kitatakiwa kuteua mtu ambaye atakuja na mwenza wake.
Nakumbuka ilishatokea, nadhani uchaguzi wa 2010 mgombea urais wa chama fulani alifariki uchaguzi ukasimama.

Sijui kwann mleta mada hakutaka kupekuwa mitandaoni!
 
Akifa nafasi ya Rais itajazwa na Makamu na swala la ugombea wake litasimamiwa na sheria ya tume ya Uchaguzi ambapo chama kitateua mwingine na siku za kampeni kuongezwa

2010 Mgombea Mwenza wa Dr Slaa Mzee Jumbe alifariki tarehe ya Uchaguzi ikasogezwa mbele kwa siku kadhaa

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Kwa upande wangu hili suala nililifikiria baada ya kuona nguvu kubwa Rais alikuwa nayo wakati na yeye pia ni mgombea. Mizani haikuwa sawa, nakumbuka kuna watu wakaibua hoja humu ya ulinzi na hata magari ya serikali yalipokuwa yanatumika kwenye kampeni. Hoja za wengine zilikuwa kwamba bado ni Rais!

Kwenye uhalisia wa mambo na yote tuliyoshuhudia, hivi Lissu angeshindwa kuendelea na kampeni wiki moja kabla ya uchaguzi, unadhani kweli uchaguzi ule ungesimamishwa hata kama sheria inatamka hivyo?

Mleta mada ana hoja ya msingi sana.
 
Kww msingi huu hata wanaodai katiba wanafuata tu mkumbo maana hata hii iliyoo hawaifahamu kabisa
 
Kigoma na Tabora ziko Kanda ya Magharibi.
Kanda ya Ziwa na idadi ya Majimbo yake:-
1. Mara - 7
2. Mwanza - 7
3. Geita - 6
4. Kagera - 9
5. Shinyanga - 6
6. Simiyu - 7
Point of correction
Mkoa wa Mwanza majimbo yake ya uchaguzi ni 9 na sio 7. Wilaya ndio 7.
Hapa chini nimeainisha majimbo ya uchaguzi mkoani Mwanza.
1. Nyamagana
2. Ilemela
3. Magu
4. Sengerema
5. Buchosa (Wilayani Sengerema)
6. Ukerewe
7. Kwimba
8. Sumve (Wilayani Kwimba)
9. Misungwi
Ikumbukwe, Mwanza ina Wilaya 7 kati ya hizo Sengerema na Kwimba zina majimbo mawili kila mmoja..

Kama Zanzibar wanaingiza wabunge 50; kwa size ya eneo na idadi ya wakazi wa Z'bar, hao jamaa wanapiga bao kweli kweli
 
Hii ni mada fikirishi ila katiba imetoa mwongozo mzuri, na tunaweza kuchukua two cases kama rejea.

Kama 2015 mgombea wa urais wa CCM angefariki maana yake JK angeendelea kuwa seating president na CCM walikuwa na nafasi ya kuamua SSH agombee kama Rais dhidi ya EL wa CDM au CCM wangekuwa na mikutano maalumu ya CC, NEC na Mkutano mkuu kuona nani angeweza kusimama na EL na wengine waliokuwa kwenye game.

2005 aliekuwa mgombea wa makamu wa Rais kwa CDM alifariki katikati ya race, uchaguzi ulisogezwa mbele na Rais Mkapa aliendelea ku-govern majuma kadhaa mpaka uchaguzi ulipofanyika na JK kuapishwa Nov badala ya late October kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kama ingetokea JPM aliekuwa seating president akafariki katikati ya race 2020, maana yake SSH alitakiwa kuapishwa ili kumalizia muda wa JPM mpaka the next president atakapopatikana kwenye uchaguzi wa 2020. Pengine CCM wangepima maji kama SSH ambae ni angekuwa seating President kama angeweza kuchuana na TL, BKM na wengine au wangelazimika kuitisha mkutano mikutano maalum ya CC, NEC na Mkutano mkuu ili wateue mgombea ambae wanaona anaweza kuwavusha kwa wapiga kura.

Nadhani hoja hii inafikirisha na tuombeaneni uzima na afya njema kati yetu; ikitokea kuna kudra za mwenyezi Mungu, basi vingunge kwenye vyama husika wangeamua nini kifanyike.
 
Katiba inaelekeza/ndiyo iliyoweka hiyo demotion kwani imesema huyo Rais ambaye alikuwa Makamu kabla kifo cha Rais, kwamba ANAWEZA kuteuliwa kugombea.
Ni ibara ipi unarejea ili twende tukasome nasi tupate maarifa.
 
Your point of correction taken. Kwahiyo ni Majimbo 43 kwa 222.
 
Good solution kichama, ila Katiba ya nchi iko silent.
 
Mkuu, majibu yako yana mashiko. Rais mstaafu anaweza kushika nyadhifa zingine lakini siyo za ndani ya Ikulu au Cabinet siyo?.
 
Mkuu, akishaonja utamu wa asali atakubali kuachia kirahisi bila shinikizo la Katiba? Ukumbuke amepewa mamlaka ya kuamuru majeshi.
 
Mkuu umekurupuka kujibu kitu ambacho hakijaulizwa na mfano wako hauna mzani mlinganyo

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, atakubali kuwa rais kwa siku hizo chache tu? Wakati anaamuru majeshi? Na pia anayo mamlaka ya kufuta/kuahirisha uchaguzi? Hapa ndiyo maana tunatafuta kujuwa Katiba inasema nini ili haya yasije kutokea.
 
Mwaka 2005 mgombea mwenza wa Freeman Mbowe alifariki dunia zikiwa zimebaki siku 15 uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi ulisimama kwa siku 28 kwa chama kuteua mgombea mwenza mwingine kisha tukaendelea na kampeni kama ilivyoada.

Kama unakumbuka uchaguzi wa 2005 haukufanyika October kama ilivyozoeleka.
 
Mwaka 2005 mgombea mwenza wa Freeman Mbowe alifariki dunia zikiwa zimebaki siku 15 uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi ulisimama kwa siku 28 kwa chama kuteua mgombea mwenza mwingine kisha tukaendelea na kampeni kama ilivyoada.

Kama unakumbuka uchaguzi wa 2005 haukufanyika October kama ilivyozoeleka.

Ila ccm walitumia mwanya huo kutoa rushwa hatari kwenye zile kampeni za nyumba kwa nyumba zilizaliwa hapa, ccm walikuwa walipita majumbani mwa watu usiku wakigawa chupi, kanga, viberiti, chumvi, mafuta ya kula na 5000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…