Ukimya wa Katiba ya JMT Kuhusu Kifo cha Mgombea Urais

Hamna mada fikirishi hapa ni uvivu tu wenu wa kutafuta maarifa....mgombea urais akifariki kwenye kampeni zoezi zima linaitishwa upya Chama kitatakiwa kuteua mtu ambaye atakuja na mwenza wake.
Watu hawasomi, na hawafuatilii matukio ya nchi, 2005 lilitokea hili analoongelea mtoa mada na uchaguzi ulisimama.

Uchaguzi hausimamiwi na katiba bali ni sheria ya uchaguzi

Mleta mada anazungumzia uchaguzi wakati hajui hata sheria na taratibu za uchaguzi.

Watanzania tumejaa ujuaji sana
 
Mkuu Matuja uko vizuri, ila hapo kwenye para ya 4, vipi kama chama kina uhakika kuwa aliyeapa kuchukuwa nafasi ya marehemu aliyefariki kwenye kampeni hauziki kwa wapiga kura alafu wakaitisha vikao hivyo kumtokosa ugombea wa urais wakati ameishaonja tamu ya urais alafu akawaza kuwa si mimi ndiyo ninaamuru majeshi? Si mimi ndiyo nina mamlaka ya kuahirisha/kufuta uchaguzi? Kwanini nikubali kuachia urais na kurudi kugombea kama running mate alafu nije nirudi Ikulu ambayo tayari nimeishakuwa rais lakini nirudi humo kama Makamu wa Rais? What is chama after all? Si ni wawahi viongozi wa chama kwa kufuta uchaguzi wote alafu naunda chama changu nakisajili na ndipo niitishe uchaguzi mkuu baada ya muda hukooo?

Mkuu Matuja, tupe maarifa.
 
Kama ni wa upinzani, moja kwa moja anakuwa amejitoa kwenye kampeni na kama ni wa CCM kampeni zinasitishwa na mgombea mwenza anakuwa mshindi ili kumfariji kwa kufiwa.
Hapana mkuu sheria iko wazi juu ya hili uchaguzi utasimama.
 
Kumradhi mkuu, alikuwa Mgombea Mwenza wa Mbowe au wa Dr. Slaa?
 
Kwa mazingira hayo mtu si unaweza kuwa raisi mda mfupi halafu ukawa makamu wa raisi kama chama kitaamua kuteua mgombea raisi mwingine halafu wewe wakakuacha kama mgombea mwenza,kama nimeelewa sawasawa.
 
Mkuu vipi kama akigundua kuwa chama kinampendekeza mwingine kuwa mgombea urais na yeye ambaye tayari ni rais arudishwe kugombea umakamu na ameishaonja utamu wa urais alafu akaamua kufuta uchaguzi, akaunda chama chake na kuruhusu uchaguzi baadaye hukoooo ili agombee kama rais? Tusaidie mkuu.
 
Hao ndo wanahitaji katiba yaani akilala katiba akienda haja ndogo katiba ili hali hata hii iliyopo hawaifaham lakin ni wajuaji balaa
 
Haya ni mambo ya vyama kama hajavinj sheria kun shida gani
 
Hao ndo wanahitaji katiba yaani akilala katiba akienda haja ndogo katiba ili hali hata hii iliyopo hawaifaham lakin ni wajuaji balaa
Msomi tufundishe unawezaje kutenganisha Katiba na Sheria? Kipi kinamuelekeza mwenzie cha kufanya? Aidha, ninajuwa kuna maelekezo ya Katiba kutaka sheria zifuatwe lakini matumizi hayo ya sheria km entity yanapoleta mtafaruku je, Katiba inakaa kimya?
 
Hao ndo wanahitaji katiba yaani akilala katiba akienda haja ndogo katiba ili hali hata hii iliyopo hawaifaham lakin ni wajuaji balaa
Mleta mada ni Mpinga katiba mpya fuatilia mada zake nyingi
 
Kwani kuna wakati taifa linakosa Rais wa nchi ikiwa kwenye uchaguzi? Rais wa nchi anafahamika wakati wote wa uchaguzi labda Rais wa nchi akifa wakati wa uchaguzi - chama kinapewa muda gani wa kuchagua mgombea mwingine.
 
Mwaka 2005,uchaguzi ulisogezwa mbele baada ya kifo cha mgombea mwenza wa CHADEMA
 
Kanda yote ya ziwa ina wapiga kura kama 25% tu. Hiyo asilimia inamwongezea tu kura mgombea lakini haina uwezo wa kuamua mshindi.

Sijui kwa nini wakati wa Magufuli watu walidanganywa na kuaminishwa kuwa kanda ya Ziwa pekee inaweza kuamua juu ya kura za Rais. Ujinga ni mzigo.
 
Mbona mwaka 2005 ulisimamishwa?
 
MIMI NINAVYOELEWA INAPOTOKEA RAIS ALIYEPO MADARAKANI AKIFA AKIWA KWENYE KAMPENI NI KWAMBA KWANZA TUELEWE KUWA RAIS KUWA KWENYE KAMPENI MAANA YAKE MUDA WAKE WA KUKAA MADARAKANI UMEISHA HIVYO IKITOKEA KIFO NI KWAMBA TUME YA UCHAGUZI ITASITISHA KAMPENI KWA WAGOMBEA URAIS TU (MAANA YAKE KAMPENI ZINGINE YA UBUNGE NA UDIWANI ZITAENDELEA) NA CHAMA HUSIKA ITAPEWA NAFASI YA KUTAFUTA MGOMBEA MWINGINE NA ASKISHAPATIKANA KAMPENI ZITAENDELEA KAMA KAWAIDA. kama kuna mwenye uelewa zaidi wa hayo mambo anaweza kutusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…