Ukimya wa Katiba ya JMT Kuhusu Kifo cha Mgombea Urais

Mkuu Douglas, ngoja tubaki ni assumptions za sasa; hizo zingine waswahili wanasema ingakuwa ngumu "kumesa".
Wakubwa wa chama au wale wanaofahamu vema falsafa za utamaduni wao wanaweza kutupa dondoo nini kinaweza kufanyika
 
Uelewa wako ni mzuri na inawezekana ndiyo utaratibu uliopo kwenye ground. Mfupa mgumu ni huu:-
Ikiwa Makamu Rais ambaye ni Mgombea mwenza atachukuwa kiti cha Rais, lakini akawa hauziki kwa wapiga kura (hawezi kuleta ushindi) kwa maana kwamba chama kinamtaka asigombee Urais, je, atakubali ugombea mwenza ili aje awe Makamu cheo cha zamani kabla hajarithi kiti cha Rais? Yaani alikuwa Makamu Rais, akapanda akawa Rais (kupitia kifo cha Rais) alafu arudi kuwa Mgombea mwenza ili aje arudie cheo cha zamani cha Umakamu, ni rahisi hii? Na kama siyo rahisi Katiba inatoa ufumbuzi upi? Kama Katiba iko kimya je, hawezi kutumia ukimya huo kufuta uchaguzi, kupiga marufuku shughuli za kisiasa kwa kiwango kikubwa? Akaunda chama chake alafu akiishaweka mizizi anaitisha uchaguzi?
 
Tatizo limeanzia hapo uliposema kama.
kama hunauhakika usipinge jiridhdishe kwanza afu uje na data halisi.
 
Inawezekana ukawa umezaliwa miaka ya hivi karibuni. Uchaguzi wa 2005 uliahirishwa siku moja kabla ya siku ya uchaguzi baada ya mgombea mwenza wa CHADEMA kufariki. hivyo katiba yetu iko wazi kwenye hilo
 
Vipi? kuna mwingine tena anafuatia maana hoja hii leo imejadiliwa saana.
 
Ilo ulilotaja hapo juu linawezeshwa na ubovu wa katiba iliyopo sasa.Hizo unazoziita dola na jamii yake vinakua hivyo vilivyo kwasababu kuna katiba inampa mtu mmoja mamlaka yakuteua hao wote.Kwahiyo kamwe usidharau katiba kama hujui imempa nguvu rais aliyepo madarakani nguvu kiasi gani.
 
Mkuu mbona hiyo inaeleweka wazi tu kwa kila mtu, ndiyo maana nikasisitiza kwamba kwa nguvu alizonazo "who can dare him/her" hata kama wewe ni Kanda ya Ziwa? Mfano, Uhuru Kenyatta alisuswa Jimbo lote la Nyanza kwenye rerun ya Oktoba 26, 2017 ambayo hasimu wake Raila aliwahamasisha watu wa Nyanza kususia rerun kwa sababu IEBC haijatekeleza makubaliano ya mabadiliko lakini pamoja na Nyanza kususa haikumzuia Uhuru kuwa rais. Pamoja na Raila kujiapisha bado haikumzuia Uhuru kuwa rais na leo Raila amekubali nguvu ya taasisi hiyo akajirudi kuungana naye Uhuru. Kwanini? kwa sababu taasisi hiyo ya rais inampa nguvu kubwa ya turufu juu ya watu na taasisi zote. Hivyo dhana kwamba Kanda ya Ziwa inaweza kuikwamisha nchi ni dhana ambayo siyo Empirical.
 
Mkuu, muda wa Rais hauishi kwa kuwa Rais yupo kwenye kampeni. Ndio maana hata wakati wa kampeni sio Tanzania tu, duniani kote, seating president anaendelea kuwa na huduma zote na mamlaka yote kama Rais, mpaka pale Rais mpya anapochaguliwa na kuapishwa.

Kikatiba Rais huwa anakoma kuwa Rais baada ya Rais mwingine kuapishwa au kama ambayo kifo kitaweza kutokea akiwa kwenye kampeni. Ni vema tuwe na uwelewa wa pamoja kwenye hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…