#COVID19 Ukiniambia kwanini napinga ripoti ya Tume ya CORONA, majibu yangu ni mepesi kabisa

Wamekula posho zao kirahisi mnoπŸ™
 
ile ripoti ni nyepesi kama unyoya, yaani hata darasa la 7 anaweza iandika.
 
Huyu mwenyekiti wa hii kamati ya covid 19 si ndiye aliyetumbuliwa na Mwendazake baada ya kupimwa mapapai yakakutwa na corona!!
 
Good analysisi
 
Kama ingekuwa ni awamu ya tano nisingeshaa kama tume hii hii ingekuja na kusema kwamba malimao, tangawizi na kujifukiza ni bora kuliko chanjo na pia hakuna corona.
Tena tume ingekuja na vitabu zaidi ya 10 vinene kuliko biblia
 
Tatizo wewe mshana jr. Kuna mapendekezo ulikuwa nayo kichwani ulitegemea yangefanana na yale ambayo yangetolewa na tume,Ndiyo maana tume imetoa mapendekezo yanayofanana na yale ya WHO,unaonyesha Hali ya kuyashangaa.
 
Hakika hili janga la corona linalazimishwa hapa nchini,wanaoshabikia hatua zinazochukuliwa na mataifa mengine no wazi wanafaidika kwa namna moja ama nyingine.
Bila aibu kamati ile inapendekeza serikali iangalie uwezekano wa kufungia watu(lockdown)
 
Umelenga Bull's eye
 
Unasema tume ime copy & paste riport ya WHO wakati hata wewe maswali mengi kwenye hii thd ni copy & paste ya maswali ambayo yameshaulizwa kuhusu Corona,umekopi mpaka misemo ya kina Einstein,Malisa GJ,

90% ya hii thd ni copy & paste ila lile kundi lako litakuja kukusifu na kukuita great thinker.

πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Mkuu umemaliza kila kitu ila sidhani kama watakuelewa.
 
Mkuu umemaliza kila kitu ila sidhani kama watakuelewa.
Mkuu nimefanya kazi za elimu ya Afya kwa umma kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa, nimefanya field yangu kitengo cha chanjo Dodoma mwaka 2016 na nimeingia mpaka kwenye wodi za wazazi.

Kiukweli hakuna watu wanaopata tabu kama watu wanaojihusisha na elimu ya afya kwa umma.

Hapo kila mtu ana imani yake.

Binafsi nakumbuka tulishawahi kuruka madirisha na kulikimbia gari la msalaba mwekundu enzi shule ya msingi baada ya kutokea uvumi kuwa hilo gari linatembea na watu wananyonya damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…