Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
- Thread starter
-
- #61
Haya ndio maamuzi sahihiUnakuta mtu hadi pete ya ndoa ananunua kwa michango ya watu. Sasa unakuta watu wanatoa kwa manung'uniko weee....unadhani hiyo ndoa itatoboa hata mwaka?? Mimi siwezi kuchangisha senti ya mtu aisee. Bora nisifanye sherehe kabisa.
MchunguUKWERII HUU
Hata mimi huwa nawashangaa watu wanataka kumridhisha nani? unakuta mtu anafunga ndoa baada ya harusi anatumbukia kwenye umaskini mkali.Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi
Imekuwa kero sana.Hili swala la kufanya harusi nje ya budget ya muhusika inabidi asasi za kiraia zianze kulipinga.
Wewe kama una laki 5 tumia hizo kukamilisha ndoa yako
Upo sahihi kabisa Mkuu.Kuna jamaa aliniganda kutaka Mchango wa Harusi nikagoma kuchangia kwasababu Mimi wakati ninafunga Ndoa Sikutaka kumchangisha kwa kuhofia kumsumbua,Sasa hata salamu hamna.Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.
Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?
Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.
Inabidi umuelimishe tu atakuelewaUpo sahihi kabisa Mkuu.Kuna jamaa aliniganda kutaka Mchango wa Harusi nikagoma kuchangia kwasababu Mimi wakati ninafunga Ndoa Sikutaka kumchangisha kwa kuhofia kumsumbua,Sasa hata salamu hamna.
Shida yule Jamaa sio muelewa.Inabidi umuelimishe tu atakuelewa