Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi

Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi

Unakuta mtu hadi pete ya ndoa ananunua kwa michango ya watu. Sasa unakuta watu wanatoa kwa manung'uniko weee....unadhani hiyo ndoa itatoboa hata mwaka?? Mimi siwezi kuchangisha senti ya mtu aisee. Bora nisifanye sherehe kabisa.
Haya ndio maamuzi sahihi
 
Ni mawazo ya kimasikini,, kwasababu pia hata nchi yetu bado ni masikini....

Michango ni scam,,, ni tumewekewa utamaduni flani ambao nafikiri dhamira yake ni kutufanya tubakie na umasikini wetu...

Kanye west aliwahi kusema "Black people wa USA wamezongwa na utamaduni wakifanikiwa kununua vitu vya thamani,, magari,na ambavyo sio vya msingi,,, LAKINI hawanunui vitu kama ardhi...

Sisi utamaduni wa michango pia unarudisha sana watu nyuma kwa sababu una involve hisia"nisipochanga hawatanichangia",,, na imekuwa mbaya mtu hujachanga unaweza hata urafiki ukaisha kabisa.,, au hujachanga harusi,,basi hakuna jambo jamii hio itakusaidia hata kama ni tatizo la ghafla...

But all in all kila mtu afanye vile nafsi yake inamtuma... Usiwe forced na external factors...
 
Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi
Hata mimi huwa nawashangaa watu wanataka kumridhisha nani? unakuta mtu anafunga ndoa baada ya harusi anatumbukia kwenye umaskini mkali.
 
Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.

Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?

Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.
Upo sahihi kabisa Mkuu.Kuna jamaa aliniganda kutaka Mchango wa Harusi nikagoma kuchangia kwasababu Mimi wakati ninafunga Ndoa Sikutaka kumchangisha kwa kuhofia kumsumbua,Sasa hata salamu hamna.
 
Back
Top Bottom