Junior. Cux
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 5,319
- 3,786
Wazimu unataka kunipanda, na nnavojijua wazimu wangu ukinipanda hata nguo ntavua.
Weekend imeenda vizuri tuu niko pembezoni mwa bahari alone akaja jamaa mmoja hv akaanza kuniimbisha. Haikuwa na shida tatizo ni MC sana yaani msema chochote mie akaniboa nikamlia kobis nikaingia JF ili aondoke. Hee macho kodo yuko sister na wewe uko JF, unatumia ID gani na blah blah kibao, nikaona isiwe tabu nikainuka kuelekea kwenye ndinga niishie kumbe alinifatilia kwa nyuma kuniona naingia kwenye gari akaenda mbio kwenye gari lake aniwahi getini. Nafika getini nataka kutoka naona range sports jeusi limeblock geti na limewasha taa zahazard kupiga honi aanatoka jamaa aliyeniboa. Alinisalimia kisha akaingia kwenye gari na kurudi nyuma kwa nguvu akanigonga. Gari yake haikuumia ila yangu ilibonyea bonnet, akashuka kwenye gari nikiwa na hamaki akanitupia kibunda cha dola mia mia chenye noti 20. Kisha akaniambia sku nyingine usilete nyodo kwa watu wenye hela halafu akaingia kwenye gari akaondoka. Yaani nilipandwa na hasira na wazimu hata nikataka kutembea bila nguo. Pamoja na kujua una range umeniboa wala hujanishawishi na pesa zako. Najua umo humu na utaisoma hii kaa ukijua lazima nikutibue.
Wazimu umenipanda Kasinde nivue nisivue...
ndo ukaniacha kwenye mataa we mtoto