Mh hivi jamani hamna yoyote anaye muonea huruma mke wa ndoa ambae ndiyo kasalitiwa?
mke amlaumu mumewe 100%, mie kila cku nasemaga mtoto chini ya mwanangu wa pili cmpokei kwenye familia yangu, nalea niliemkuta alienikuta inamuhusu na baba yake na mama yake na uzinifu wao, kila mtu abebe mzigo wake aise.
nilimpeleka mtoto hosp for a check up maana alikuwa na ka-homa kidogo! Wakati nasubiri kuingia kwa daktari nikasikia kelele za kilio toka chumba kingine, mama/dada mmoja akawa analia "nataka mtoto wangu, nipe mtoto wangu"
kwa makadirio ya haraka mimi na wateja wengine wa pale hospitalini tukahisi kwamba yule dada/mama alikuja na mtoto mgonjwa na either amefariki au kuna kitu kibaya kimetokea!
Mara tukasikia tena kelele za kuomba msaada "ananiua, ananinyonga", ikabidi tukimbilie kwenda kuona nini kinatokea! Tukakuta doctor mwanaume ambaye tshirt yake imelowa damu anamkaba yule mama sakafuni, wakaachanishwa!
Sasa baada ya ile sakata kutulia, yule dr akaingia kufanyiwa dressing ya wounds za kisu nyuma ya kichwa na shingoni!
Ikabidi tutafute sababu ya yule mama kumjeruhi yule dr ambaye tulidhani ni mume wake, kumbe ni tofauti kidogo! Yule mama aliongea kwa uchungu sana, akatueleza kwamba yeye na yule dr walikuwa ni wapenzi,
huyo dr ana mke na watoto sita wa kike, sasa amezaa na yule nyumba ndogo mtoto wa kiume! Yule jamaa akakata mahusiano na yule dada, mtoto alipofikisha mwaka 1 na miezi mitatu yule dr akaja akamchukua mtoto on mother's absence
akaenda kumficha anakojua! Sasa ndo yule mama akaja kudai mtoto pale kazini kwa hawara yake/baba mtoto! Dr akam-provoke kuwa yeye hakuwa na shida na yule dada, alikuwa na shida na mtoto wa kiume, so achape lapa! Dada wa watu ndo akawa mbogo, dr akaanza kumdunda, dada akatoa bisu lake akampa za shingoni na utosini!
Je wapendwa wazazi wenzangu, ingekuwa wewe ungeweza kuchukua uamuzi kama huo?
Ulianza kwa ku-generalize issue.... hebu tuendelee kujadili % ya watoto wanaozaliwa katika ndoa na kulelewa na baba na mama kisha wakawa na staha. Na je, mfano baba na mama wameoana mmoja wao au wote wakiwa na watoto tayari, wakawalea kwa pamoja, inakuwa staha au sio staha?
Baba habebi mimba. Mmefanya ngono kwa starehe zenu (na kwa kupenda kwenu starehe mkaona inakuwa tamu zaidi bila condom), na wewe mama unaelewa uwezekano wa mimba, bado unataka kichapo cha live, sasa kama si kujibebesha mimba hapo ni kufanya je?Kwani umejitia mimba mwenyewe?? Baba yupo ndo maana mimba ikaingia na sio kwamba baba anazuiwa kuja kumuona mwanae...
Hiyo ni tofauti maana hata mtoto atakuelewa kuwa hukuwa na nia ovu, ni bahati mbaya ilitokea baada ya kuzaliwa. Si kama yule anayepanga kuzaa kwa kumkosesha mwanaye baba.
Nakubaliana na wewe kwa hili, mtoto ni mtoto especially ukiwa mama, lazima utamfeel mtoto yeyote...
Niliwahi kumzaba kibao mama mmoja pale saba saba... alikuwa na watoto wawili ambao wamepishana kama miezi tu au mwaka... ametoka nao ndani ya maonyesho, watoto wamechoka vibaya sana, it seems walikuwa na njaa pia, and it was late around 7pm, akawa amembeba yule mdogo na anamburuza yule mkubwa... kale katoto kakawa hakawezi ku-keep pace na mama yake, kakawa kanaumia na kanalia, yule mama akaanza kumfokea na kumpiga... aisee i felt a twinge, nikajikuta nimemzaba kibao... lakini kumbe wengi walikuwa wanamwangalia anavyofanya ndo wakaanza kumgombeza, kwanza kwa nini amekuja na watoto wadogo hivyo kwenye fair grounds wakati anajua hali halisi ya pale... kwa kweli niliumia...
So, sio wamama wote wako hivyo, if a mother can desert his/her child then hashindwi kumfanyia mtoto wa mwenzie... inategemeana na roho ya mtu!! Ndio maana kuna malaika na shetani
Sasa ulivyogeneralize kwamba wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi wakati kuna ambao wanazaa kisha wanaachana?
naona una matatizo ya uelewa. Wapi niliposema wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi? Nimesema na narudia tena, wanawake wanaozaa watoto na wanaume ambao hawana ndoa nao wanafanya tabia ambazo hazina tofauti na zile za mbuzi wanaokutana machungani au mbwa koko wanaokutana majalalani maana wale hawana maadili, wanajizalia tu. Sijasema wazazi wote, acha uzushi.[/QUOTE]
HE!!!!!!!!!!!!!!!!
naona una matatizo ya uelewa. Wapi niliposema wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi? Nimesema na narudia tena, wanawake wanaozaa watoto na wanaume ambao hawana ndoa nao wanafanya tabia ambazo hazina tofauti na zile za mbuzi wanaokutana machungani au mbwa koko wanaokutana majalalani maana wale hawana maadili, wanajizalia tu. Sijasema wazazi wote, acha uzushi.[/QUOTE]
HE!!!!!!!!!!!!!!!!