TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Mwanaume ukioa Moshi/Kilimanjaro unakua tu ni sawa umeolewa maana kila mwisho wa mwaka wakwe na mashemeji wanaporudi kwao kwa ajili ya sikukuu na wewe utakua unalazimishwa kwenda.
Nina ndugu zangu 4 wameoa Kilimanjaro, wafanyakazi wenzangu na marafiki zangu na watu wengine ninaowafahamu ambao sio wenyeji wa Kilimanjaro ila kila inapofika mwisho wa mwaka lazima waende huko.
Hata Pascal Mayala amesema yeye kila mwisho wa mwaka huenda Moshi wakati ni Msukuma wa Kanda ya Ziwa.
Ukioa Moshi ni kama umeolewa wewe maana utapelekeshwa kama mbuzi.
Anyway, haya ni maoni yangu na mtazamo wangu, sio lazima uyapende.
Mleta mada unaonekana hujui chochote kuhusu mila za wachaga. Katika jamii nyingi za wachaga, mwanamke akishaolewa haruhusiwi tena kurudi na kulala nyumbani kwao unless kuwe na tatizo kubwa kama msiba ndio ataweza kulala. Mwanamke anaeweza kurudi uchagani na kulala ni yule ambae hajaolewa. Kwahiyo hao unaoona wakienda uchagani ni wanaume wa kichaga ambao aidha wameoa wachaga wenzao au wameoa makabila mengine. Kamwe mwanamke wa kichaga hawezi kumchukua mume wake halafu akamlaze kwa baba mkwe uchagani maana yeye mwanamke haruhusiwi kulala huko!