Ukioa Kilimanjaro unakuwa ni sawa na umeolewa wewe, kila mwisho wa mwaka unatakiwa kwenda Moshi sherehe za mwisho wa mwaka


Mleta mada unaonekana hujui chochote kuhusu mila za wachaga. Katika jamii nyingi za wachaga, mwanamke akishaolewa haruhusiwi tena kurudi na kulala nyumbani kwao unless kuwe na tatizo kubwa kama msiba ndio ataweza kulala. Mwanamke anaeweza kurudi uchagani na kulala ni yule ambae hajaolewa. Kwahiyo hao unaoona wakienda uchagani ni wanaume wa kichaga ambao aidha wameoa wachaga wenzao au wameoa makabila mengine. Kamwe mwanamke wa kichaga hawezi kumchukua mume wake halafu akamlaze kwa baba mkwe uchagani maana yeye mwanamke haruhusiwi kulala huko!
 
Wewe ni muongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke.wa kichaga akisha olewa hata chumba chake wanapangisha mwingine
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli hata Mimi kananivutia,natamani sikukuu moja na Mimi niende moshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekaa K'njaro nimesoma na wachaga, my best friend baba yake na mama yake ni wachaga. Baba yake alimwambia mwanae asioe mchaga, from this nikapigia mstari msimamo wangu uliokuwepo. Sitoutaja hapa nisije onekana nina chuki
 
Mchaga yupi? Kuna wamachame, warombo, wamarangu, wauru, wakibosho, waoldmoshi na wote hao wanalugha zao hawasikilizani kabisa. Ndugu zangu wameoa wamachame na wamarangu na bado wanaenda huko na kulala kwa wakwe! Au wewe unasema mambo ya mwaka 47?
 
Inawezekana kukawa na ukweli kwenye hili maana kuna baba mkwe wetu ni mtu wa kanda ya ziwa mama mkwe wetu ni mchaga ila mara kwa mara mwisho wa mwaka mzee anakuwa Kilimanjaro sio kwao
 
Umalaya sio kabila ni tabia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…