Ukioa mke mkirsto mkatoliki una asilimia nyingi za kuwa na familia yenye furaha na mafanikio

Ukioa mke mkirsto mkatoliki una asilimia nyingi za kuwa na familia yenye furaha na mafanikio

Oooooohooooh baba usituletee matatizo huku. Hawa wanawake wetu wa kikatoliki muwaache kwanza hawana mapepo na huku hatuna mambo ya mapepo usije ukatuletea walokole huku wakatuletea majini ya mwamposa.

Hebu mtuache. Kwanza nikasali novena sasa hivi.
 
Halafu kwann waislam wakiingia ukristo na ikatokea wakasilimia kanisa katoliki huwa ni ngumu sana kurejea kundini yaani Islam? [emoji848][emoji848]
 
Yaani siku zote umekaa na hii siri bila kutupa wenzako hii code? ngoja nianze na hii parokia ya mtakatifu agusto。
 
Nipe ratiba za misa zenu
Jumatatu hadi ijumaa
Saa 12:15 alfajiri hadi saa 1:00 NA
Saa 10:30 hadi saa 11:00 jioni

Jumapili
Misa l saa 11:00 alfajiri
Misa ll saa 12:30 alfajiri
Misa ll saa 2:30 aubuhi
Misa lV saa 4:30 asubuhi
Misa V saa 10:00 jioni

Kuabudu ekaristi takatifu saa 11:00 jioni

karibu
 
Hiyo jinsia wote wanafanana... Wakiwa ndani ya ndoa kwa ufupi desa lao ni moja regardless ..dini au kabila
Jibu la ukweli liko hapa, kwingine kote porojo tu.

Tena ingekuwa siyo one size fit all basi wanawake wa kiislamu ndio wangekuwa wanawake bora kabisa kwa jinsi ya muongozo wa dini yao unavyowataka kuwa.

Bila mihemko na kashfa za kidini dini ya kiislamu ndio dini bora kabisa katika mafundisho ya jinsi mke anatakiwa kuwa vipi.
 
Kupitia mifano mingi hawa wanawake wa kikatoliki ni bora sana kujenga familia sio Tanzania tu hata duniani.

Mzee wangu ni muislamu alioa mke mkatoliki.

Mama alikataa kwenda kwenye uislam akabaki na ukristo wake lkn familia ilikuwa na amani na furaha sana.

Tulipokuwa primary hatimae mzee wetu naye akaenda kanisani mpaka sasa ni mkatoliki.

Sijawahi kusikia hata siku moja wakigombana wakati tunakua.

Mama hakosi jumuiya, hakosi kanisani, hakosi tukio lolote la kijamii kanisani.

Nimejaribu kuwaza nje ya familia, familia nyingi za kikatoliki zimenyooka sana sio Tanzania hata duniani.

Wanawake wakikatoliki kwanza hawayumbishwi kiimani.

Sisemi 100% kwamba wakatoliki wote lakini namba kubwa inawasapoti.
Kijana!

Duniani kila MTU ana pair yake,bila kujali Imani au dini aliyonayo mtu!

Ukiipata pair yako hata akiwa mpagani mtaishi TU na mta match na chemistry itaendelea Hadi uzeeni!

Tatizo ni pale tunapotumia Dini kama kigezo Cha mahusiano yetu bila kujali ni pair Yako ya asili!!?

Kuna watu wameoa wrong people coz ya udini na viceversa is true!

Pair yako ni ipi!!?
Usimkatae mtu kisa dini yake we zingatia je mkikaa mnaekewana!!?mnapendana!!?

Hivyo tu!
 
Naunga mkono hoja Hawa wadada wa kilokole ni shida sana wanapewa mafundisho ya hovyo sana na hao manabii wao na kukuona mume wake kama shetani tu.
 
Jumatatu hadi ijumaa
Saa 12:15 alfajiri hadi saa 1:00 NA
Saa 10:30 hadi saa 11:00 jioni

Jumapili
Misa l saa 11:00 alfajiri
Misa ll saa 12:30 alfajiri
Misa ll saa 2:30 aubuhi
Misa lV saa 4:30 asubuhi
Misa V saa 10:00 jioni

Kuabudu ekaristi takatifu saa 11:00 jioni

karibu
Asantee
 
Back
Top Bottom