Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Usipoweka mipaka mwanamke wako hatokuheshimu. Na mwanamke asipokuheshimu hawezi kukupenda. Wengi wapo kwenye mahusiano yasiyo na mapenzi. Sababu mwanaume hana mipaka. Ukiwa na mipaka mwanamke anakuona we una thamani zako. Sio wa kuendeshwa na mwanamke.
Kama ukiweka mipaka na mwanamke wako. Ukajieleza vile unataka muishi. Lakini hapendi, tambua ya kuwa hiyo ni shida yake na sio tatizo kuhusu wewe, au ubadilike ufanye kitu usichokitaka ili umridhishe au umfanye ajisikie furaha.
Ukiona unapata shida kuweka mipaka ujue kuna kitu unaogopa. Aidha, Unaogopa kumpoteza huyo mwanamke, au unaogopa atakunyima mapenzi, au unaogopa ukimkosa huyo hutopata kama yeye tena, au
Unaogopa utamfanya ajisikie vibaya na atakosa furaha. Hutaki akasirike. Unajiona kuwa wewe ndo una jukumu la kuhakikisha anajisikia vizuri kila muda. Ujue ndani yako kuna ujasiri umekosa. Pengine unaona hauna haja ya kuweka mipaka sasa, mana baada ya muda mambo yatabadilika. Sio kweli.
.
Cha kufanya:
Anza kueleza unavyojisikia bila kuchuja maneno.
Mwanzoni utahisi unaweza kumpoteza mwanamke. Au, kama ulimzoesha kukuendesha naye atakushangaa maana ni kitu kipya. Lakini mwisho wa siku atazoea au ataondoka. Ujipange kwa lolote. Tambua mwanzoni itakua ngumu utajiona unakosea lakini endelea kujizoesha.
Ongea na wanawake wengi zaidi.
Ni kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kujieleza vile unavyojisikia. Itakusaidia pia kuwa na mbadala kama mwanamke wako wa kwanza hatokubaliana na mipaka mipya uliyomwekea. Pia, utajitengenezea ujasiri na kujiamini zaidi kwamba mwanamke hawezi kuwa juu yako, na akiondoka sababu ameshindwa kuishi kwenye mipaka yako basi ni hasara yake mwenyewe.
Usije ukajiumiza kwa ajili ya mtu mwingine kwa kuvumilia kitu ambacho hukitaki. Mfano mdogo, unamtongoza mwanamke au uliyenaye mapenzi yenu yamepungua na mwanamke wako anaanza kukuita bro/ kaka/ muhuni wangu/ mshkaji/ ndugu, ukimuachia ataona huna tofauti na wanaume wengine huko nje anaowaita majina hayo na hufai kimapenzi. Hivyo usivumilie, wala kuogopa kumsahihisha ukiamini baadaye mambo yatabadilika ukishamfanya akupende.
Pia wakati unaweka mipaka usitumie njia ya kuzunguka kuelezea kile unachotaka kusema. Kiseme vile unavyojisikia bila woga. Kwa kutumia mfano hapo juu, usiseme “mh nimekua ndugu tena, unajua ukimuita mtu ndugu bla bla bla(unaanza kujitetea kwanini usiitwe ndugu/ mshaji)” badala yake unaweza muimbia tu “usiniite ivo, chagua majina mazuri ya kuniita”.
Huo ni mfano mdogo tu lakini ni muhimu uweke mipaka ya jinsi unavyotaka kuishi na mwanamke. Chukulia kama vile yeye ni maji anaenda uelekeo wowote atakaojisikia lakini wewe upo kama mkondo wa maji, wewe ndo unaamua uelekeo.