Ukiombwa leseni ya gari na ukatoa bila kiambatanisho, imekula kwako!

DON YRN

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Posts
606
Reaction score
1,453
Wale mabwana wana njaa hatari, hata buku buku wanachukua. Ole wako utoe leseni bila kiambatanisho utaulizwa hadi "herro, kwa nini tairi za gari yako zina vumbi?, nakuandikia kosa.

Ukiombwa leseni, toa na kiambatanisho baadaye utakuja nishukuru nimekaa pale!.
 
Tumeshajua kwamba una gari swala la kutoa rushwa inaonyesha ulivyo maskini gari halijakamilika.
 
Kama unaendesha gari ya million 15 kushuka chini we tayari una makosa inabidi uwe mpole haijalishi umelipia kila kitu na umeweka tairi mpya kitendo cha kuwa na IST tayari umevunja sheria za barbarani
 
Na wale mabwana hata hawana muda wa kuangalia kama hii pesa ni feki
 
Lazima uwe na Fotocopy ya CV na Academic transcript ili wajue wewe ni msomi au wewe ni mweupe
Sijawahi ona uzwanzwa wa kiasi hiki barabarani! Sidhani kama kuna mtu ambae hayupo timamu kiasi hiki barabarani labda kama leseni umenunua!

Udereva ni taaluma tofauti na taaluma nyingine ni inajitegemea na ndio maana kuna watu wamesoma na wanaelimu kubwa na bado wanaajiri madereva wa kuendesha hivyo vi babywalker vyenu

Ukifikia hatua hiyo barabarani ujue kabisa bado hujafikia kukaa barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…