Ushauri kwa madereva wenzangu, hakikisha unaongea nao politely, na usiruhusu mazingira ya rushwa. Wewe weka ngumu hata akisema anakuandikia fine sema sawa. Mimi nina matukio 3.
1 . Mataa yalizimika katikati yaani nilipita na taa za njano nikasimamishwa, wa nyuma yangu akaachwa, walijizungusha kama nusu saa hivi wanabishana nani aongee nami, yaani wanakuja wanaondoka mi niko friendly kabisa sijashuka, ikabidi mmoja aseme anaenda ofisini, akabaki mmoja hana hata ujasiri wa kuniandikia akisubiri nitoe chochote (bila kudai ila mazingira yalijionesha kabisa anasubiri nitoe kitu na sikutoa) nani nikakaa kimya nasubiri afanye maamuzi.
2. Damage ya taa ile cover ilikuwa imepasuka kidogo sana unaweza hata kucheka yaani ni mpaka usogelee ndo utaona, taa inafanya kazi poa tu, akanisimamisha eti gari yako iko sawa ila shida ni hiyo taa, na waliiona baada ya kusimama maana ilikuwa ya nyuma, nikasema shida iko wapi mbona inawaka na ni cover tu imepasuka hapo pembeni , akajizungusha eti nakuandikia fine nikasema sawa afande, akaondoka, anakuja tena mara ya pili nakuandikia fine au unasemaje, nikasema sawa afisa maamuzi ni yako, akaondoka, kaja mara ya tatu kanipa leseni eti ukaitengeneze nikasema niko kwenye process hata hivyo.
3. Mwingine akanisimamisha ananiomba elfu 5 ya supu, eti we ni mtu wa kwanza kukusimamisha nipe elfu 5 basi nikanywe supu, sina kosa na hajakagua gari wala nini, just like that, ila kuna maafisa wa polisi watachomwa moto wenye petrol ndani yake.
Wanakera , you just need time ⏲ acha waste wanachotaka bila kuvunja sheria wewe tulia maana hawakawii kukupakazia kesi nzito ukajikuta lockup,
Kuna dereva wetu ofisini alisingiziwa kutaka kumkanyaga polisi, in reality hakuna kitu kama hicho kilitokea maana nilikaa passenger seat ya mbele na niliona tukio lenyewe,
It was like this: alimsimamisha dereva akawa hajui kama kasimamishwa yeye au we nyuma yake, tukapita tukibishana namwambia simama kakusimamisha wewe akasema hapana siyo mimi, kapunguza mwendo kaona mwenzie wa nyuma kasimama, dereva wetu akaendelea na safari nikamwambi utakutana na kizuizi traffic wa mbele na ikawa hivyo, kilichonishangaza ni kidai alitaka kumgonga wakati alisimamisha magari akarudi pembeni hakukuwa na anything close to incidence ya kunusurika kugongwa, wenzake wakapiga simu na kuweka loudspeaker, jamaa akawa anasema kabisa "ndiyo alitaka kunigonga huyo, mpaka sasa sijatulia akili yangu maana nimenusurika kifo", yaani criminal case kabisa!
Kwq kifupi wanacheza sana na woga wetu, ni mara mia nilipe fine, bora ikasaidie kujenga taifa kuliko nilazimike kumlipa mtu ambaye ananifanya miye kitega uchumi chake kwa lazima. Maskini jeuri miye.