Mikono yenye Sugu
Senior Member
- Jul 1, 2020
- 133
- 215
Ghafla umezuka wema kutoka kusikojulikana kuwaomba CHADEMA wawasilishe majina ya wabunge wa viti maalum ili wajumuishwe kwenye mchakato wa uapishaji.
Hii inaogopesha! Ni wiki moja tu imepita tokea wafuasi na viongozi wa CHADEMA kufanyiwa kila aina ya unyama na mwisho kupokwa kila walichostahili kwenye zoezi la uchaguzi.
Cha ajabu kuna jitihada kubwa sasa za kuwabembeleza wachukue nafasi ya viti maalum "vya kugawiwa" na waliopora kila kitu.
Tahadhari kwa CHADEMA; ukiona adui anakubembelezea chakula au maji, chukua tahadhari. Huenda chakula hicho kimetiwa sumu, ama ya kukuua ghafla au ya kukumaliza polepole.
Msishiriki haramu iliyotendeka kwa ahadi ya peremende, matajimaliza wenyewe.