Ukiona hujakipata ukitakacho elewa bado hujakitaka haswa. Ulimwengu unatoa chochote atakacho mtu.

Ukiona hujakipata ukitakacho elewa bado hujakitaka haswa. Ulimwengu unatoa chochote atakacho mtu.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Katika hali ya kustua ni ukweli kuwa tumekuwa na tabia ya kujiridhisha na kujiliwaza kuwa tumetiabidii sana ila hatujayapata tuyatakayo lakini uhakika ni kuwa hatujataka haswa tuyatakayo.

Ulimwengu una kila tunachotaka na unaweza kutupa ila ni mpaka tutake haswaa. Hakuna mtu aliyetaka kitu kwa dhati akakikosa. Tusijiliwaze tu kwa kutamani na kuishia kusema tumekosa. Kujitahidi ni zaidi ya kusema "nimejitahidi sana ila bado", hakuna aliyeuonesha ulimwengu bidii juu ya akitakacho akakikosa.

Kutamani kitu chochote ni ishara kuwa ulimwengu unaweza kukupa kitu hicho ukikihitaji lakini kuhitaji kitu hicho siyo tu kutamani kukipata ila ni kuhakikisha unakuwa kitu hicho kwa kutoa nguvu zako bila kukoma "bidii isiyokoma".

Hapa namaanisha kutokurudi nyuma Kwa sababu yoyote ile. Ni kule kuendelea hata kama kuna kila hali ya kukatisha au kukatishwa tamaa. Unapokuwa katika hali hiyo hakika Ulimwengu utaachilia tu kile unachohitaji.

Siandiki haya yote Ili kumtia mtu moyo au matumani la hadha! Ila ninachokilenga ni kumtaka mtu kuelewa tu kanuni za asili za ulimwengu na kukwepa kivuli cha kujiliwaza " comfort zone".

Hakuna npatakayekuonea huruma usipojionea huruma wewe juu ya kupata uyatakayo. Uyatakayo unayeyajua ni wewe, hivyo anayepaswa kuwajibika hakika ni wewe na siyo mtu mwingine yeyote. Kumbuka kuwa wewe ndiye dereva haswa wa maisha yako.

Kukata tamaa kwa tasfsiri nyepesi ni hali ya kuridhika na mazingira yalivyo na kuacha kuendelea " kukubaliana na hali". Hakuna sehemu ambayo wanadamu wengi tunapakimbilia Ili kujiliwaza kama eneo la kukata tamaa. Kukata tamaa ni kama mti mkubwa wa kivuli cha watu wengi.

Hakika na hapa sijitoi, ninajisema na Mimi mwenyewe kuwa kukata tamaa ni chaguo la mtu binafsi anapokupali kukosa anachokihitaji na Hilo halimaanishi anachokihitaji hawezi kukipata. Au niseme tu wazi kuwa wengi wetu kati ya kupata na kukosa tunachagua kukosa.
 
Back
Top Bottom