Pre GE2025 Ukiona imefika mahali Freeman Mbowe akaja na kampeni ya Samia Must Go, basi ujue amechoka sana na mambo ni mabaya mno

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Freeman Mbowe ni mwanasiasa mtulivu, mwenye werevu na uvumilivu mkubwa sana. Hadi imefika Mbowe anaamua kuwa Samia Must Go, basi ujue kwa kweli mambo hayaendi vizuri katika nchi hii na kuna tatizo kubwa mno.

Pamoja na kwamba uvumilivu ni jambo jema sana kila wakati, kuna mahali inafika hata vitabu vitakatifu vinatuambia kuwa ...yatosha sasa.., kuna wakati wa kucheka na wakati wa kukasirika..

Tuwaunge mkono wote wanaokasirishwa na mambo ya hovyo yanayoendelea katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na ukatili dhidi ya watoto, kutekwa na kuuwawa kwa wanasiasa na wanachi wengine, na usimamizi mbaya wa rasilimali za Taifa letu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'
 
Eti wanajitekenya kweli?
 
Ni mtu mwenye busara ila haibasilishi ukweli kwamba samia tunae hadi 2030
 
Hata paka akichokozwa sana, mwishowe hugeuka kuwa chui.
 

Your browser is not able to display this video.
 

View attachment 3094294
 
Uvumilivu huwa una mwisho, binadamu akichoka kuvumilia matendo yake hubadilika kabisa.
 
Mbowe anatumia haki ya kidemokrasia. Na hii ndio tofauti ya Samia na wengine watano waliomtangulia.

Samia ana akili pana sana. Nasikitika kusema ukweli kwamba hizi ni harakati zitakazozimwa kama za enzi zile za nyuma.

Tatizo la Mbowe ni kukosa ubunifu wa kisayansi na pia huu ni ushahidi wa elimu yake kuwa duni, huwezi kutumia mikakati ile ile iliyofeli siku za nyuma ukategemea ije ikupe matokeo chanya kwa wakati unaokuja.
 
Mbowe na vijana wake wa mitandaoni anaowalipa kwa kazi ya kusambaza chuki, wakati kile anacholipwa na mfumo kinakuwa ni kikubwa zaidi.

Mchaga kwa akili ya kutafuta pesa he is always second to none.
 
Kweli amechoka miaka 21 chama hakina mafanikio!
 
Mbowe na vijana wake wa mitandaoni anaowalipa kwa kazi ya kusambaza chuki, wakati kile anacholipwa na mfumo kinakuwa ni kikubwa zaidi.

Mchaga kwa akili ya kutafuta pesa he is always second to none.
Steve wewe haya yanayoendelea ni kama unapaswa mafuta tuu. Ila kuna watu mna roho ngumu
 
Posho imechelewa tu ndo anapiga kelele,
Mkwe mwenye chama anangoja chake kule kijijini.
Asali haijapatikana kama inavyotakiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…