Pre GE2025 Ukiona imefika mahali Freeman Mbowe akaja na kampeni ya Samia Must Go, basi ujue amechoka sana na mambo ni mabaya mno

Pre GE2025 Ukiona imefika mahali Freeman Mbowe akaja na kampeni ya Samia Must Go, basi ujue amechoka sana na mambo ni mabaya mno

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Freeman Mbowe ni mwanasiasa mtulivu, mwenye werevu na uvumilivu mkubwa sana. Hadi imefika Mbowe anaamua kuwa Samia Must Go, basi ujue kwa kweli mambo hayaendi vizuri katika nchi hii na kuna tatizo kubwa mno.

Pamoja na kwamba uvumilivu ni jambo jema sana kila wakati, kuna mahali inafika hata vitabu vitakatifu vinatuambia kuwa ...yatosha sasa.., kuna wakati wa kucheka na wakati wa kukasirika..

Tuwaunge mkono wote wanaokasirishwa na mambo ya hovyo yanayoendelea katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na ukatili dhidi ya watoto, kutekwa na kuuwawa kwa wanasiasa na wanachi wengine, na usimamizi mbaya wa rasilimali za Taifa letu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'
Hana influence hata chamani
 
Steve wewe haya yanayoendelea ni kama unapaswa mafuta tuu. Ila kuna watu mna roho ngumu
Nimeyaona haya miaka ya nyuma na naujua mwisho wake utakuwa vipi.

Kuna kazi kubwa ya kutafuta wawekezaji iliyofanywa na Samia, na hivi sasa nchi nzima michakato ya kujenga viwanda vikubwa inaendelea haswa mkoa wa Pwani.

Hizi zote ni fursa pana ambazo Samia kazitafuta mwenyewe kwa kwenda huko nje, zile faida za safari za Samia zinaanza kuzaa matunda na yatakuwa makubwa.

Mbowe alitakiwa aione hii vision na ukubwa wake na aje na mikakati ya kusaidia vijana wa chama chake na sio kuwatumia wakiwa ni mtaji wa kufanya siasa zenye nia ya kuichafua serikali.

CHADEMA na wadau wasioridhishwa na serikali ya sasa wanapaswa kutafuta uongozi mpya utakazisimamia sera na mwelekeo mzima wa upinzani
 
Kweli amechoka miaka 21 chama hakina mafanikio!
Sera ni zile zile za wanaharakati za kuja na matamko yenye siku fulani ya kufanya kitu fulani. Siku inapita anakuja na kauli mbiu nyingine yenye siku maalum ya kufanya kitu fulani na mara nyingi yanakuwa ni maandamano.
 
Back
Top Bottom