Ukiona kwenye mkutano wamejaa wanaume!! Ogopa sana

mkokamoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2024
Posts
1,313
Reaction score
1,671
Kwenye mikutano mingi ya kisiasa wanawake na watoto hususani wanafunzi huwa ndo wengi zaidi huku ni nadra kukuta kundi kubwa namna hii la wanaume

CCM na serikali yake wana la kujifunza hapa, watu wanatembea kwa miguu wengine umbali wa zaidi ya kilometa mbili,

Hawajasombwa kwa magari au maroli bila kulazimishwa na yeyote ila tu kwa sababu ya uzalendo walionao kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania wamejitokeza kuisikia #no reforms no election

CCM cheche zimeshaanza kuonekana mkisubiria sana bila kukubali mabadiliko ndo tuende kwenye uchaguzi mkuu moto utawaka mwaka huu👿
 
Wanaume huwa wanatumia akili zaidi, ndio maana mpango wa kuwaingiza chaka wapambane na serikali unakwama. Wanabaini uongo mapema.

Unaweza kuwapanga eti mkavamie msitu wenye simba au mkavamie hifadhi ya nyuki, watakusikilizaaa weee, halafu siku ya tukio huwaoni! Afanaleki.

Cc: Kisutu kwa Lissu
 
Hakuna cha moto kuwaka
 
Bila kushiriki uchaguzi ni kazi bure.
 
Uzuri mikutano ya wapinzani haina chawa wale wasanii wa mama
Kwenye mikutano ya upinzani hoja zao ndo zinajaza umati ila kwa CCM bila wasanii na kuwasafirisha makada wao huwezi kuta watu👿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…