Ukiona Mnanda unakumbuka nini au wapi?

Ukiona Mnanda unakumbuka nini au wapi?

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Binafsi inanikumbusha mwaka 1979 mjini Njombe alikuwepo Afisa Utamaduni mmoja aliitwa Sapali aliitumia kuburudisha kwenye sherehe mbalimbali za kiserikali na chama tawala, vilevile mjini Iringa alikuwepo mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi Igangilonga kama sikosei sana alikuwa anaipiga kwa umahiri kwenye sherehe mbalimbali

1645602435620.png

My take:

Kuna hatari ya kizazi kilichopo na kijacho kushindwa hata kupiga ngoma
 
Naionaga kwenye taarabu za wazanzibari
 
Unaujua mnanda?? Hio ndio sababu uliitwa mnanda.
 
Naionaga kwenye taarabu za wazanzibari
Sawa Mkuu lakini zipo za aina tofauti hii design ni tofauti hii ya juu ipo kama typewriter😄
1645613260545.png

1645603105457.png

Wazanzibari wanapiga hizi👇
1645603150831.png
 
Enzi hizo nikiwa na imani kamili,nilikuwa sikosi kuhudhuria mikutano ya mzee Mosses kulola,kulikuwa na mwimbaji mmoja wa nyimbo za injili akiitwa mzungu four,huyu mtu alikuwa anakigandamiza hicho kifaa hadi unahisi usingizi,alikuwa sambamba na Faustine munishi,umenikumbusha mbali.
 
Sasa hivi una Imani nusu?
 
nimemkumbuka mzee Mayagilo,enzi kanisani Mkalapa na kwenye masherehe ya ndoa akiwa na kundi lake la kwaya.
 
Nakumbuka matukio ya ukabaji na uporwaji Wa mchana kweupeee!! Huko maeneo ya temeke mikoroshini, Tandika n.k Wahuni wamevaa vipensi tu na ndala zimewekwa mfuko Wa nyuma!
 
Nakumbuka matukio ya ukabaji na uporwaji Wa mchana kweupeee!! Huko maeneo ya temeke mikoroshini, Tandika n.k Wahuni wamevaa vipensi tu na ndala zimewekwa mfuko Wa nyuma!
Ndio ilikua zao,kama sikosei ile style ya uimbaji walikua wanaita mchiriku,wanapita group wanaimba na kupiga huo mnada huku wanapora watu.
 
Nakumbuka matukio ya ukabaji na uporwaji Wa mchana kweupeee!! Huko maeneo ya temeke mikoroshini, Tandika n.k Wahuni wamevaa vipensi tu na ndala zimewekwa mfuko Wa nyuma!
🤣
😂😅😆
 
Back
Top Bottom