Ukiona mtaani Gari zimeandikwa katika Plate Number kama ifuatavyo usiumize kichwa

Watu mna moyo. Hii kazi yote hii mnapata wapi nguvu ya kuandika kwa mapana hivi ilhali sio business kwamba unapata kipato?
Ndo shida ya wabongo hii, yaani wewe unawaza hela tu???? Hivi unafikiri pesa ndo kila kitu? Hujui kuna watu humu wamejifunza kupitia uzi huu?

Kuna watu wamejifunza humu ili wakafundishe hata watoto wao ambao wako darasa la saba huko mashuleni wakasome na kujibia mitihani ya MAARIFA YA JAMII au mkuu hujui kuwa kuna vijana wetu ambao wanahangaika kusoma huko ili wapate hicho kipato unachokisema?

Maisha si kama unavyoyaona mkuu, wapo wengine wako bookly oriented, let them add something in their cabotio, kipato kipo tu hata wewe ukiulizwa swali kati yako wewe na mtoa hoja nani ataonekana bogus???

Wewe unayejua kuwa andiko lake halina muktadha wa kipato ndo uneonekana kituko, umepoteza muda kujibu ujumbe ambapo ungekuwa unaingiza kipato hahahahaha. Maisha baanaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi safi nlikua nafanya kazi kwenye miradi ukoo Basi nakaa pale najitawala kwa Kupanda DFP land cruiser wala sikujua maana ake iyo DFP tulitamba sana kwa road uko vijijini daa🤣🤣
 
1. Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
Namba za magari yanayitumika kumbeba Rais au Makamu wa Rais na Waziri Mkuu haziandikwi namba wale herufi katika kibao chake, bali huwa na nembo ya taifa ya Bwana na Bibi. Kwa Kiingereza magari haya hufahamika kama State Cars.

2. Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
Spika wa Bunge pia gari lake huwa halina namba kwenye kibao chake bali huwa na herufi S pekee. Gari la Naibu Spika nalo huwa na herufi NS pekee. Maana ya herufi S ni Spika na NS ni Naibu Spika

3. Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatumia gari ambalo lina kibandiko chenye herufi CS pekee. Ikiwa maana ya CS ni Chief secretary

4. Jaji Mkuu wa Tanzania
Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake, Jaji-Mkuu

5. Mkuu wa Majeshi (CDF)
Gari la Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kibao chake huwa hakuna namba wala herufi zozote bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake

6. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
Magari ya Waziri na Manaibu wao huwa na herufi zinazoonyesha cheo (kama ni waziri au Naibu waziri) halafu hufuatia ana vifupisho vya majina ya Wizara zao. Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake

7. Gari za Serikali za Mitaa
Magari ya Serikali za Mitaa, yanayotumiwa kwenye Serikali hizo. Magari hayo kuwa na kibao chenye Herufi SM zikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Serikali-mtaa

8. Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO). Kibao chenye namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.

umoja-mataifa

9. Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
Magari ya Ubalozi nchini Tanzania huanziwa na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba. Pia namba hizi hutumiwa na wafanyakazi wa ubalozi husika hata kama ni Watanzania. Mfano wa Ubalozi ni Marekani

balozi-jpg.

10. Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
Magari yanayotumiwa na mashirika ya Umma huwa na kibao (Plate Number) ambazo huanziwa na herufi SU na kufuatiwa na namba tofauti tofauti kwenye vibao hivyo

shirika-umma

11. Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu to nje ya nchi
Magari yanayotumika kwenye miradi inayofadhiliwa kutoka nje ya nchi kuwa na kibao chenye herufi DFP (Donor's Fund Project) ikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Pia tofauti na DFP utakuta mengine yana DFPA

12. Magari ya Police wa Tanzania
Magari ya Polisi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi PT (Polisi of Tanzania) halafu hufuatiwa na namba tofauti tofauti mbele yake

13. Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania
Magari ya Jeshi la Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na namba kadhaa kisha hufuatiwa na herufi JWTZ kisha hufuatiwa na namba tena.

14. Magereza Tanzania
Magari ya Magereza ya Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi MT kisha hufuatiwa na namba kadhaa mbele yake kwenye kibao cha magari hayo

15. Serikali ya Tanzania
Serikali ya Tanzania ina gari zake tofauti tofauti ambzo hutumika kwa mfano Wilayani au hata kwenye halmashauri. Magari haya huwa na kibandiko chenye Herufi za mwanzo STK au STJ au STL na baada ya hapo hufuatiwa na namba kadhaa mbele

16. Magari ya Wakuu wa Mikoa
Wakuu wa mikoa wote nchi huwa na magari ambayo huwana plate number ka tofauti. Gari la mkuu wa mkoa huwa na kibandiko ambacho kuanza na herufi RC na kisha hufuatiwa na herufi ambazo ni kifupi cha mkoa wake. Herufi RC humaanisha Regional Commisioner. Mfano; RC NJB- Mkuu wa Mkoa Njombe

17. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Serikali ya mapinduzi Zanzibar hutumia magari yenye kibao chenye kuanziwa na herufi SMZ kisha kufuatwa na tarakimu kadhaa. Magari haya hutumika kwenye shuguli za kiserikali hivyo hupewa viongozi wa serikali katika ngazi fulani

18. JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa

19. JK- Jaji Kiongozi

20. J- Jaji wa Mahakama Kuu

AG - Attorney general huyu mwanasheria mkuu wa serikali

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. CAG - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

23. Magari ya watu binafsi
Magari ya watu binafsi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanza na herufi T kisha tarakimu tatu hufuata na baada ya hapo herufi tatu hufuata. Magari haya ya binafsi yanaweza kuwa ya biashara au la.

Pia kwenye magari ya binafsi ambayo sio ya biashara kunauwezekano kuwa na kibandiko ambacho kina jina mtu binafsi.

NYONGEZA:
Magari yote haya huwa pia na tofauti katika rangi za plate number hizo, rangi hizo zinaingiliana sehemu na sehemu;

1. Magari yenye plate number za Rangi ya Njano Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake Katibu Mkuu Kiongozi Jaji Mkuu wa Tanzania Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali.

Gari za Serikali za Mitaa

Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
Serikali ya Tanzania Magari ya Wakuu wa Mikoa

2. Magari yenye plate number za rangi ya Kijani

Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
Magereza Tanzania

3. Magari yenye plate number za rangi nyeusi

Magari ya Police wa Tanzania (Maandishi ya rangi ya njano)
Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (Maandishi ya rangi nyeupe)

4. Magari yenye plate number za rangi nyekundu

Mkuu wa Majeshi (CDF) (Nyota zilizopo huwa na rangi ya dhahabu)
Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu toka nje ya nchi

5. Magari yenye plate number za rangi nyeupe

Magari kwa ajili ya biashara (Commercial Use)
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

6. Magari yenye plate number za rangi ya bluu
Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa.
Mkuu tuwekee na picha tuone
 
Umesahau CGI (Commissioner General of Immigration) UT (Uhamiaji Tanzania)
 
Maelezo mazuri ahsante...

Kuna mdau mmoja alishauri kwanini gari za umma zisiwe zinatoa lift kwa wananchi pale panapokua na shida ya usafiri mf ..Dar...ili kuleta ile maana ya Mali ya Umma lol😅
 
Back
Top Bottom