Ukiona mtaani Gari zimeandikwa katika Plate Number kama ifuatavyo usiumize kichwa

Tofauti ya 8 na 9 sijaelewa halafu... nimecheka uliposema eti number plate rangi ya njano ni marufuku kwa biashara wakati Kibongo bongo unaeza kuta gari na hiyo nembo ya taifa lakini inapigishwa zake ruti za kupeleka watu mnadani kula nyama[emoji38][emoji38][emoji38]
 
naomba nitoke nje ya mada kidogo. mi nauliza tu kuna zile gari unakuta mbele kwenye bonet, zina kama kibendera cheusi, maana yake ni nini!?.. au mtu yeyote anaweza kukiweka tu
 
Gari za Uhamiaji zinafupishwaje kwenye plate number?
 
Gari za Wakurugenzi wa Halmashauri huwa na number plate nyeusi na yaananza na herufu mfano SJX, SJL
Hacha izo, bora ungekaa kimya ...... hizo ulizo zitaja wala hazitumiwi na halmashauri uliza vizuri wanao elewa watakuambia nani wanatumia hizo plate number. Magar ya halmashauri yanaanza na SM (serikali ya mitaa). So na gari la mkurugenzi wa halmashauri ni SM.....
 
Na ile MMM na SG ni za nani,
Alafu kuna hizi zenye namba za Singapore nazo ni za tasisi gani plate namba nyeusi na maandishi ya silver.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Jamaa wala hajakosea . Tangu kipindi cha uchaguzi Wakurugenzi wanatumia hizo namba zilizokaa shagalabagala au wengine wanatumia namba za kawaida kabisa yani T XXX XXX ,nafkiri ni kwasababu ya kuficha identity

Ila kikawaida yes Halmashauri zinatumia SM
 

Unabisha kwa sababu hujawahi kuona. Nikae kinya kana kwamba nimeandika ujinga au😀. Acha ubinafsi, kwa hiyo unalolijua wewe ndiyo ukweli pekee?

SJK, SJX etc kuna namba kama hizo.

Sema kwa sababu ya kulinda heshima siwezi kutaja Halmashauri yenye namba kama hizo.
 

CPA anabisha asichokijua. Au kwa kuwa tupo nyuma ya keebody anadhani tuna level sawa ya kufikiri na kuona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…