Wakuu Ni Vyema Na Haki ushauri wako ukajikita zaidi katika kujenga na kuboresha Familia yako.
Sio sahihi kutoa ushauri kwa mtu usiyekuwa na mchango wowote ule katika uchumi wake kama hajakuomba umshauri.
Nitajikita sana kwa wafanyakazi wa mgodini maarufu kama Miner.Hawa watu wanasemwa sana kuwa wana mishashara mikubwa ila wanaitumia kwa Ana's. Nikweli mishahara yao iko vizuri.
Kwanza unapaswa ujue mgodini jitihada zako za kujua machine mbalimbali ndo zitakufanya uwe na mshahara mrefu zaidi. Mzawa kulipwa milioni 30 sio jambo la kushangaza nikawaida sana.
View attachment 3275466
Hii hutegemea anajua machine ya Aina gani na ina kazi gani.
Sasa ukiwa Expert mshahara wako wa mwezi mmoja tu ukiachana na bonus unaweza ukajenga nyumba nzuri ya kisasa na ikaisha.
Mfano chukulia expert alipwe $35k utakubaliana namimi kibongobongo nyumba ya kisasa unajenga na inaisha.
View attachment 3275465
Ukweli ni kwamba Kazi za mgodini ni ngumu sana na very risk mno imagine kuna migodi unazama shimoni km2 au zaidi.
Hewa inaletwa kwa machine hadi mliko na kuna baadhi maeneo sio rafiki kabisa (kuna mgodi una km2 na mita6) ukienda Decline unakuta na joto la hatari ukiwa umevaa rainboot au gambuti Zina jaa maji
Zile deli za maji Lita 5 unainywa kwa masaa2 inaisha na hapo yawe ya barafu umeweka mabonge ya barafu.
View attachment 3275484
Chukulia hewa inayokuja/unayovuta ni ya joto. Lakini eneo hilo utapaswa uwepo shift nzima yaani masaa zaidi ya 6 una tinga pale!!
View attachment 3275468
Huko underground ni sawa na kuzimu hakuna usiku au mchana. Kuna giza Totolo ambalo wewe hujawahi fikilia utakutana nalo. Kiasi kwamba taa yako ikizima hutaweza kuona kitu chochote hata ukipitisha mkono wako mbele ya macho yako hutaweza kuona kitu.
View attachment 3275479
Kwa maana hiyo basi itakupasa utembee huku ukiwa umeshika ukuta hadi Access (njia kuu) ili iwe rahisi kupata msaada.
Ukiwa unatembea ujue ukuta ule wote una wire mesh nazo zimesha haribiwa na machine ni very risk vibaya mno.
Ni ngumu sana kuelewa au kuelezea kwa mtu ambae hajawahi fanya kazi mdogino hasa Underground.
View attachment 3275469
Unaweza ingia na msosi na usipate muda wa kuula kabisa hadi ukarudi nao au ukaishia kuutupa tu!
Wengi wa wafanyakazi Afya zao ni hatarishi hasa migongo,kiuno nk
Hii ni kutokana na ku operate machine au barabra nk.
View attachment 3275467
Hayo ni baadhi tu ya mazingira ya kule kwa kifupi sana. Hela unaipata kwa jasho na damu halafu mtu akae kijiweni kukujadiri kuwa wafanyakazi wa migodini hela wanatumia ovyo sana kwenye starehe!!
Sioni tija yakutoa ushauri kwa mtu usiyechangia kitu chochote kile kwenye uchumi wake mbaya zaidi hajakuomba ushauri wako.
View attachment 3275464
Mimi kila nipatapo nafasi na wenzangu au tukikutana na walio nje na niwe mapumziko kukesha siku2 mfurulizo ni kawaida kabisa.
Kazi hizi ni ngumu mno kama una bishi waulizeni watu wa idara ya madini wanao shuka ardhini na hao wote huko chocho huwa hawapelekwi na hawataweza kupelekwa kule!!
View attachment 3275463
Nina matukio kadhaa ya mimi kunitokea wakati nikiwa kama jumbo Offsider (Driller Assistant)..........Nilizimia chanzo joto kali,
Nikiwa nimeshika mesh op alininyanyua juujuu pamoja na mesh(hapo alikuwa na jumbo single boom)
Jingine nikiwa kama Long hole offsider......Niliteteleza nikaning'inia operate hakuweza kunivuta mwenyewe ikabidi akaombe msaada hadi wanakuja nipo nimening'inia kama dk35!!Nimewahi vunjika kidole na mengine mengi.
View attachment 3275471
Yapo matukio makubwa na mengi sitayasema hapa.
Punguzeni ushauri