Ukiona siri za jumba jeupe zinavuja, basi hiyo ni taa nyekundu kwa kiongozi wa nchi

Genge la Bashiru walitaka wamuweke Majaliwa kwahiyo asingepata hata hiyo miezi mitatu bila Mabeyo.
Sasa unaona mkanganyiko huo?
Kwa upande mmoja, akina Mabeyo wanasimamia kwenye taratibu za Katiba, na kwa upande wa pili, genge likiwa radhi kukiuka hata hiyo katiba mbovu!

Matokeo yake ndiyo haya tunayo yashuhudia sasa; na tutaendelea kuyashuhudia sana chini ya taratibu zilizopo sasa.
 
Mi naamini huyu ndiye atakaye leta mabadiliko yasiyo tegemewa, hata kama ni kwa njia ambayo hatukuitegemea itatufikisha huko kwenye mabadiliko hayo.

Kama Tanzania itashindikana kubadilika chini ya uongozi wa Samia; sijui kama kutakuwepo na mabadiliko tena. Maana yangu ni kuwa Samia ndiye atakaye kuwa sababu ya mabadiliko hayo.
 
Kwa maslahi ya Taifa, na kwa maslahi ya taifa tu wakati mwingine inabidi kufanya maamuzi magumu kuchagua lesser of two evils.

Katiba yenyewe sasa hivi inaheshimiwa unaona yanayoendelea kwenye chaguzi za serikali za mitaa, Spika aliyepita alivyofukuzwa, sakata la DP World, misitu, Ngorongoro?

Kwa sasa neno Rais ndìo katiba yenyewe, yupo juu ya mihimili yote na katiba.
 
Watanzania bado sana, pamoja na kwamba maisha ni magumu bado wanaweza kupata ugali, pia ni waoga sana.

Nchi imegawanyika sana kupitia dini, makabila, kanda, vipato, mjini na vijijini, vyama lukuki. Hakuna umoja kwa maslahi ya Taifa.

Nchi hii inahitaji vijana kiongozi, anaweza kuiunganisha bila kujali vyama, dini, kabila, vipato, kanda nk Nchi inahitaji coalition ya vyama vyote na hata wanaCCM wenye uchungu na nchi yao kwa maslahi ya Taifa.
 
Hata sijui; hilo genge kweli liliufahamu ubovu wa Samia kuwa ni wa kiasi hiki alicho onyesha hadi hapa tulipo fikia sasa baada ya kumjuwa vizuri?
Ni nani aliye juwa kuwa angekuwa mbovu kiasi hiki alicho onyesha hadi sasa!

Bado sioni unafuu au uhalali wa hatua hiyo iliyo taka kuchukuliwa na hilo genge. Tunapotoka kwenye njia sahihi na kuchukua njia za pembeni, hilo pekee ni tatizo kubwa
 
Mimi nitakufahamisha moja kwa moja. Katika hayo uliyo yaorodhesha kwenye aya yako ya pili, "dini" sasa ni tatizo, pamoja na kwamba watu hawataki kulisemea waziwazi.
Nakubaliana na wewe juu ya uhitaji wa "kiongozi" wa kipekee kabisa kulirudisha taifa katika misingi yake ya awali.
 
Wewe unamatatizo sana, KIONGOZI siyo MUNGU. Na ikiwa ni Kiongozi, anaowaongoza wanapaswa kufahamu kiongozi wao yuko wapi na mipango yote. Akisafiri anapaswa kutoa taarifa kwa anaowaongoza, anakwenda wapi na kufanya nini, na kwa muda gani, na ikibidi awaombe ruhusa na waridhie gharama anazokwenda kuzitumia.

Uliyoyaeleza ni ya WATAWALA, amabao wao wako juu ya sheria hawaulizwi na hawahojiwi na yeyote. Na zaidi kila wafanyacho kwao ni SIRI kwasababu hawatendi wema, bali ulaghai na wizi wa mali zisizo zao.

Safari ya kiongozi haipaswi kuwa siri, na hata akiugua tunapaswa kufahamu, kwasababu UONGOZI hakujipa bali kapewa na hao anaowaongoza.
 
Tatizo lilianza walipomchagua kuwa makamu kwa vigezo visivyo na mashiko. Ni kama Democrats Biden na Kamala. Trump amejifunza sababu anaweza kufa madarakani. Amechagua at least competent deputy.

Vyama vyote inabidi vichague kwenye ticket wagombea wenye uwezo wa kuongoza, likitokea la kutokea.

Muhimu katiba ibadilishwe, sheria iwe uchaguzi mwingine ndani ya mwezi mmoja hadi mitatu. Nchi inahitaji katiba mpya.
 
Walio/wanaoSOMA vyuo wana kitu wanaita kusap yaani unaweza kuona wenzako wanatunukiwa kwenye mahafari wewe umebaki hapo.

So kama hujaelewa baki hapo kwanza muda wako bado 😁!.
Hiyo ni carry kabisa, bora angalau kupata sup 😂
 
Nyingine wanavujishaga makusudi

Ila kuna moja nzito na I verify kwanza hapa

Nzito mno!

Nilitaka nichape Uzi Ila nikagundua kuna code ziko wazi sana nikauweka pending (Draft)

Ila nikiwaza CHATU kufa wakifuatana si vema sana!
Britanicca
Fafanua kdg na sie tuelewe. Doooh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…