Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,240
Avumiliaye mpaka mwisho atauona ufalme wa Mbinguni. Sijakata tamaa bado. Sasa Chagua wewe.
Kula tano...! Kuna siku nilijisahau kuzitoa kwenye dashboard, mamsap katika pekua pekua akazikuta pale rough riders ...akaniuliza vipi tena hizi....nikawa mkali vijana wa garage hawa wajinga sana.....akaniambia inamaana wewe huwa hutumii ? Nikaishia kumwambia tuheshimiane, ila ujumbe ulinifikia!
Mpwa una bahati huna mke wa mamsap wa aina ya Carmel au Nyamayao. Lol!
Masa umeniacha hoi, yaani nimecheka mpaka kilio sasa, khaaa mie ningekubana walah mpaka kieleweke, yaani umeanza kujitutuma hivyo nikuachie?
Shangazi..hapo ndo utashangaa maana kibao atakachokugeuzia utadhani yeye ni malaika - hapo hajakukuta na kitu umempa warning tu! Msome Chrispin alipojibu kuhusu kukuta C kwa mamaa..ndo utaelewa..
Unachosema ni kweli.Kuna msemo huwa nawasikia watu wanasema ukiona kwenye gari kuna mwanamke na mwanaume halafu wanaongea na kucheka ujue hao ni mtu na kimada/nyumba ndogo.Na kama hawasemeshani yani wamenuna ,basi ujue hao ni wanandoa halisi.ZD...kwa bongo yetu wanandoa wenye mawasiliano mabovu mbona ndo wengi!
Masa umeniacha hoi, yaani nimecheka mpaka kilio sasa, khaaa mie ningekubana walah mpaka kieleweke, yaani umeanza kujitutuma hivyo nikuachie?
mimi nimekubaliana na hao.ila inabidi hili suala watu wasijue sasa.tutawa-PM ili tupate kura zao na misimamo yao.Badae tutatangaza matokeo kama yatakuwa mazuri.
Si unajua ile fomula ya wanaume usikubali hata kama utakutwa uko mtupu na mkeo/partner? Tafuta sababu yeyote ila kamwe usikubali hiyo ni sumu!
thats true Kiongozi...by the way mambo yanakwendaje mtaa wa saba hapo?
Shwari kabisa tunasikilizia uchaguzi mpya Afghanistan, Mkuu Hamid Karzai alicheza faulo kwa Abdullah Abdullah
Kula tano...! Kuna siku nilijisahau kuzitoa kwenye dashboard, mamsap katika pekua pekua akazikuta pale rough riders ...akaniuliza vipi tena hizi....nikawa mkali vijana wa garage hawa wajinga sana.....akaniambia inamaana wewe huwa hutumii ? Nikaishia kumwambia tuheshimiane, ila ujumbe ulinifikia!
ulikamatishwa ndani ya kumi nane teh teh teh
mbaya zaidi labda ulikuwa na appointment jioni yake
home kuaga tena huwezi ....
ndio maana yake, mimi nikimpata mke kama huyu nitafurahi sana halafu pia hata kumega nje itakua sio sana, kutokana na kwamba mtu ukimwacha free anaogopa kuharibu tofauti na ukimbana mkuuHehehe kwa hiyo jamaa huru kumega huyu dada anamjali sana mmewe big up sana wote igeni mfano huo jamani tutapona kwa gonjwa hili hatari.
kuna dada mmoja alikua anamwekea mumewe condom kwenye bag kila akisafairi, jamaa siku akamuuliza mkewe akamwambia wewe ni mwanaume na huko uendako unakutana na mademu kibao na tamaa inakuwepo, so ni bora nikuweke ili usije kufa kwa ngoma kuliko kujidai hufanyi, so jamaa mkewe yupo free ili kuepusha kuambukiza ukimwi
hilo sasa lipo kwa mtu binafsi, maana kuna baadhi ya watu wananzinunua kabisa lakini akifika katikati ya gemu anaivua eti anachelewa au hakuna ladha halisi, huwa wanadai utakulaje pipi na ganda lake?Kumuwekea kondom si suala muhimu hapa suala muhimu anazitumia?
Akina dada,mama, shangazi na bibi najua wote mna viburudisho vya kurusha navyo roho katika tunda la mema na mabaya....na mnavipenda kweli kweli maana mnasaidiana kwa kila kitu hata kungonoka.
Swali langu Je wewe mama au dada ukiona CONDOM mfukoni mwa suruali ya mmeo aidha wakati unafua au unapanga nguo chafu ikadondoka utafanyaje?
kama n mimi nitampongoza kwa kujijali kama mapokeo ya pongezi yangu yatakuwa mazuri nitamuuliza vipi ofisini kwenu leo mlikuwa na semina ya UKIMWI akijibu hapana ndo nitendelea na mijadala mingine hatimae ataniambia ukweli kuliko kudanganya kama mtoto mtodo eti mafundi wa gereji wameniwekea Kweli inawezekana?
Ni hayo tu wandugu
Tumsifu yesu kristo