Ukiondoa hasara ya shirika la Ndege ATCL, ni wapi tena penye ufisadi wa serikali ya awamu ya tano?

Ukiondoa hasara ya shirika la Ndege ATCL, ni wapi tena penye ufisadi wa serikali ya awamu ya tano?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Hivi, ufisadi wa JPM Ukiondoa zile hasara zilizosababishwa na ufufuaji wa shirika changa la Ndege ATCL ni wapi tena palipofanyika ufisadi mithili ya kipindi cha awamu ya nne!

Na Kwa nini ufisadi wake umechuja Kwa Kasi ya ajabu kutajwatajwa mitandaoni ili Hali bado tunakumbukia Lichimondi, EPA, Lugumi n.k ambapo ni ya kitambo Sana??

Huyu kweli alikuwa ni fisadiii...au wamemkandia??

Ile bilioni 60 ilisababishwa na hasara za kiuendeshaji ktk shirika letu la Ndege, Kwa nini uitwe ufisadi na sio usimamizi mbovu??

Ufisadi, Maana yake ni nini Kati ya pesa kupigwa na kupata hasara?

Katika wizara ya maliasili ya Wakati wa Kigwa, yeye alisema anasubiria apelekwe mahakamani kuwagalagaza,

Ni upi ufasadi wa kutisha wa Swami ya tano, au ni dili za kisiasa za watu...! Na Kwa nini tarifa hizi zichuje Kwa haraka kiasi hiki,

Ukichangia, useme ni wizara gani, ama shirika lipi la Serikali kumepigwa pesa na ni kiasi gani
 
TPA Billion za kakoko

TASAC posho hewa za mabilion

TAMISEMI Overpriced Expenditure za ukarabati na magari n.k

Kwenye SGR ripoti ya CAG inasema walilipa wakandarasi kwa inflated Forex rate ili wagawane cha juu!!

CCM ni kansa alichofanikiwa JPM ni kubana tu utoaji taarifa otherwise hta tender za Bombardier kuna 10% pale zimeliwa
 
Hela Mwendazake aliyoiba ni zaidi ya Trillion 8. Na iyo ni miaka mitatu yake ya mwanzo. Jumlisha ufisadi wote wa awamu zote hizo sijui EPA Escow haifikii wa huyu jamaa.

Ilibidi aende zake angeendelea kuishi hata zaidi ya mwezi sijui ingekuwaje.

Afe tu tena huko alipo.
 
Mkuu, unaweza kupungua kidogo chuki ili uzungumze ukweli Kwa kuthiibitisha
 
Barabara ya Ubungo Kimara ni wizi mtupu. Barabara ya hovyo haina viwango

SGR yenyewe ni wizi tu hamna kitu
 
Marehemu dikiteta magufuli alikuwa hapendi kukaguliwa matumizi ya fedha za walipakodi/wanyonge, mpaka ikapelekea kumuona cag Assad kama adui wa serikali yake, so ni obvious dikiteta magufuli alifanya ufisadi mkubwa ktk kila shirika la serikali.
 
Unaamini zile hesabu za Polepole za magazijuto zilikuwa zinatosha kuelezea yale matumizi ya Trillion 1.5 ?
 
ATCL sio ufisadi, ukiangalia kwa jicho pana utaona hasara yote ya ATCL haihusiani na JPM, madeni ya nyuma ya kabla ya shirika kufufuliwa hayahusiana na JPM, ameyakuta aliamua kutotapanya pesa ovyo kwa kulipa madeni yasiyoeleweka. Kuhusu mkataba wa ATCL na wakala wa ndege za Serikali, sioni kama ni inshu kubwa kwa ATCL kuwalipa hawa jamaa wakati ndege hazifanyi kazi, hawa wote ni serikali pesa imetoka mfuko wa kushoto ikaingia wa kulia. Ilibidi waseme pia wakala wa ndege wa Serikali ameingiza faida kiasi gani ili tulinganishe na hasara ya ATCL.
 
Huna macho? Huna masikio?
Juzi tu hapa Majaliwa aling'aka kuhusu mradi wa mwendo kasi kwamba unakufa. Je sio ufisadi, siyo hasara? Hukuona? Hukusikia?

Vipi kuhusu Mamlaka ya Bandari hadi mkurugenzi akawajibishwa? Je, sio ufisadi, sio hasara? Hukusikia, hukuona?

Kwa taarifa yako Mwamba alifanya madudu mengi zaidi ya EPA au Richmond sema alidhibiti kupekuliwa, kusimamiwa na kukokoselewa katika utawala wake.
 
Mkuu nisaidie kumuuliza maswali haya:
1. Hivi zile korosho walizoporwa wakulima pasipo kulipwa mpaka zikaozea maghalani na kupoteza soko sio ufisadi?
2. Hivi kudhulumu wafanyabiashara hata wakafunga na kuhamisha biashara zao sio ufisadi kwa taifa?
3. Hivi kujenga kwao kulikuwa ni kwa manufaa ya Taifa au ufisadi mwingine?
4. Hivi kutowapandisha daraja na mishahara watumishi sio ufisadi ama hujuma kwa Taifa?
 
Mkuu, hayo Ni matendo pengine twaweza kuyaita yasiyofaa, mada hii inataka tuanike ufisadi na wizi wa serikali yake, yaani ulaji wa fedha

Kama fedha zilijenga kitu, na hicho kitu wanatumia Watanzania ingawa ni Kwa makosa, huo sio ufisadi

Ainisha ufisadi kama ambavyo Lichimondi na EPA au Lugumi jinsi pesa zilivyokuwa ziapigwa
 
Kila mahali kuna ufisadi. Soma ripoti ya CAG vizuri. Ila Watanzania ni balaa, hawajali Rais ni dikteta uchwara au full dikteta watu wanapiga tu.
 
Jizi na genge lake walikuwa wanajilipa around 17-25 b /month kwa kuweka pigment kwenye mafuta.Malipo yakifanywa kwa kikampuni chao

Baada ya Shabiby kuwaumbua bungeni eti ndio wakadai wamesitisha mkataba.

Hapo hatujaoneshwa.jumba la kifahari la mwendazake kijijini kwao Chato hadi waandishi walipigwa biti kutuonesha fahari ya Rais wa wanyonge
 
Hela Mwendazake aliyoiba ni zaidi ya Trillion 8. Na iyo ni miaka mitatu yake ya mwanzo. Jumlisha ufisadi wote wa awamu zote hizo sijui EPA Escow haifikii wa huyu jamaa.

Ilibidi aende zake angeendelea kuishi hata zaidi ya mwezi sijui ingekuwaje.

Afe tu tena huko alipo.
Anayeiba anaweza akafanya yote hayo aliyofanya magu kwa muda mfupi ? Basi na aheri kuwa na mwizi anayeifanyia nchi maendeleo kuliko mwizi asiyeifanyia nchi maendeleo , nadhani wewe haupo Tanzania ndio maana unaongea haya , zunguka Tanzamia nzima nadhani hautarudia tena kuogea hizi pumba zako.
 
Piga kinubi Mkuu, piga saaana, hii itasaidia jamaa atafufuka very soon arudie tena kiti chake!
 
Back
Top Bottom