Kama mada kwenye kichwa ilivyo, ukimuondoa MZEE NYERERE aliyetupatia uhuru na kisha baadaye kuwa na Mzee Mkapa katika awamu ya tatu, niseme wazi Tanzania imekuwa ikongozwa na viongozi wenye uwezo mdogo na wastani sana.
Katika Uongozi, Mzee Mkapa ndiye angalau aliimarisha mifumo ya Serikali na kuweka wasomi wenye weledi katika Serikali haijatokea kama huyo tena.
Jakaya, JPM na hata SSH kwa kweli ni viongozi wenye uwezo wastani sana katika kuendesha Nchi. Kwa hali hiyo hata mifumo ya uongozi Serikalini katika awamu zao imejaa watu wa kawaida sana (below average)
Kwa msingi huo tutegemee danadana tu bila hatua zozote za maana. Itachukua muda sana kumpata MKAPA mpya wa Tanzania hii. Sioni kama ni leo ama kesho.