Kama binadamu Mkapa alikuwa na udhaifu wa kuwa mbabe au ujivuni kiasi flani. Lakini kama kuna kiongozi ambaye ingekuwa mfumo wetu upo vizuri aliyekuwa na akili alikuwa Mkapa.
Alijiamini kupita kiasi.angekuwa amejishusha kiasi flani alikuwa ana uwezo wa kuifikisha nchi mbali sana. Alikuwa na exposure, maono na kujiamini sana. Mfumo ulikuwa mwaribu. Akadumbukia ndani yake akaharib.
Mkapa alikuwa Rais ambaye unaweza ukamsikiliza ukapata kitu.aligundua kuwa he wasnt a comedian so hakuwa na muda wa kutaka kuchekesha watu kwa kuongea pumba.
Speeches zake zilikuwa kali,zenye ujumbe,kujiamini na kuongelea jambo analolifahamu kwa kina. Since then hatukuwahi pata Rais mwenye akili au smart kama Mkapa.
Nakubaliana nawe mkuu. Marehemu Ben Mkapa hata kama alikua na upendeleo kwa ndugu/marafiki zake ilikua sio waziwazi na ni vigumu sana kujua. Hakua na double standards kwenye kuwa treat watu kwa maana ya kuwabagua kwa makabila, dini zao au mahali wanakotoka
Alirudisha hadhi na heshima kwa watumishi wa umma kwa kuwaongezea maslahi kwa maana ya posho na mishahara. Hiki ni kipindi ambacho watumishi wa umma walifurahia sana ajira zao kwenye Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
Aligoma kuwapa TAKUKURU nguvu zisizo na mipaka za kukamata na kushtaki watu moja kwa moja akielewa kwamba kwa nafasi yao wanaweza wakaitumia sheria vibaya na kuonea watu. Alitaka wafanye uchunguzi kamili kwanza na wamshawishi DPP kwa ushahidi uliokamilika kabda kupeleka mahakamani ili haki itendeke
Aliondoa kodi zisizo na maana ambazo pia zilikua kero kwa ukuaji wa biashara za watu. Kwenye kipindi chake leseni za Biashara zinazotolewa na Halmashauri za Miji ilikua unalipia mwaka mmoja tu tena flat rate ya 20, 000.0 tu kwa biashara yoyote na hakuna ku renew kila mwaka!
Alidhibiti mfumuko wa bei na alihakikisha thamani ya shilingi ya Tanzania inakua imara na isiyoyumbayumba kwa kutumia njia halisi za kiuchumi
Aliijengea nchi heshima kwa wahisani na wabia/wadau wa maendeleo na aliweka wazi kabisa kwamba nchi itakua inalipa madeni yake iliyokopa. Kwa namna hii alifanikiwa sana kupunguza deni la taifa ambalo lilikua limepanda sana hasa kwenye serikali ya awamu ya pili. Hata huku kujigamba kwa serikali yetu kwamba tunakopesheka na deni letu la taifa bado ni himilivu kunatokana na misingi aliyoiweka Mkapa
Pamoja na kuanzisha wakala nyingi za serikali ambazo zikawa ni taasisi zinazojitegemea bila kuhitaji ruzuku kutoka Serikali Kuu pia miradi kama MKUKUTA na MKURABITA ilikua ni wazo zuri sana kama watekelezaji wangekua makini
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, marehemu Benjamin W. Mkapa aliitendea haki nafasi ya Uraisi na hakika ameacha alama ya uongozi uliotukuka