Ukiondoa Waziri Mkuu, anayefuata kwa kazi nzuri ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Ukiondoa Waziri Mkuu, anayefuata kwa kazi nzuri ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Sijawahi kufuatilia kwa ukaribu kazi za huyu jamaaa anapotembelea wakulima hadi nilipoona akaunti ya wizara ya kilimo huko Tiktok.

Kiukweli HUSEIN BASHE anafanya kazi nzuro sana ya kuwanyanyua wakulima! Ni vile tu Awamu ya TANO ilivuruga mifumo mingi sana hadi kwenye kilimo na hii inapelekea kilimo kuyumba kwa muda.

Ila kwa kasi anayoenda nayo Bashe I hope na naibu wake angekuwa hivi yaan mambo yangekaa safi.

Nimefurah anatatua tatizo hapo hapo mbele ya wananchi, mtu anakula hela za wakulima na bado anadunda mtaani, Bashe anakamata anaweka ndani mpaka walipe hela za wakulima! Hawa vyama vya ushirika wapumbafu sana hawa wanapenda kukaa na hela za wakulima muda mrefu mwishowe wanawaibia.

Nasema BASHE piga kazi ya Rais Samia hiyo unamsaidia sana sana sana kamata wezi weka ndani piga na viboko!

Kazi nzuri Mungu atakulinda.
 
Tatizo ni kwamba watumishi wa serikali wamerudia tabia za enzi zileee za mjomba. Bashe ana ubunifu lakini hana network zenye maadili.
 
Awamu hii wengi wanajitahidi,kina Aweso, Manaibu wa Tamisemi, Waziri wa Afya, Waziri wa Elimu, Ujenzi nk

Ila sikubaliani na PM naona Mara nyingi anagundua makosa ila anashindwa kuchukua hatua hasa kwa Wakurugenzi.

Fukuza kama anavyofanya Aweso
 
Bashe ni smart sana, tatizo yupo kwenye mfumo Ambao upo corrupted, matunda yake yamaweza yasionekane Sana
 
Mleta mada weka jina na namba ya simu ndicho ulichosahau
 
Hiyo kazi nzurii anayofanya bashe ni ipi?.au mnashawishika na zike hekaya zake za majukwaani[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Uzuri kilimo hakihitaji u mbuni,matokeo yake huwa yako waazi kabisaa.

Mtu hata swala la mbolea tuuu limemshinda, sasaa ninii ataweza?.CAN kutoka 47000 hadi100000 ni jambo la kupongezaa?.

Mbolea za ruzuku ni siasaa tupuuu.
 
Mfumo wa ruzuku ni kapu la WABENZI kujikingia kipato haramu kwa mgongo wa wakulima yanayo hubiriwa majukwaani na bashe ni tofauti na yalivyo kwa ground.

Wanajificha kwenye chaka la corona na sasaa wamehamia vita ya urusi na Ukraine. Gilba
 
Mwizi anawaibia wakulima anakamatwa kisha ana ambiwa arudishe pesa! What's next akitoka anarudi ofisini endelea na kazi!
Tuache UCHAWA wa kitoto hapo mfumo ni ule ule. Vipo wapi vyombo vya usalama kudhibiti wizi huu! Hii sio kazi ya Waziri.
 
Mwizi anawaibia wakulima anakamatwa kisha ana ambiwa arudishe pesa! What's next akitoka anarudi ofisini endelea na kazi!
Tuache UCHAWA wa kitoto hapo mfumo ni ule ule. Vipo wapi vyombo vya usalama kudhibiti wizi huu! Hii sio kazi ya Waziri.
yeye akiwaumbua kazi inayofuata ni mamlaka zingine kama takukuru na polisi kumalizana nao.


Waziri anaposema OCD kamata hawa! maana yake mamlaka ziendelee na mambo ya kisheria
 
Wa Tz tujifunze kutofautisha kazi nzuri na matangazo ya maigizo ya kazi nzuri.

Anachofanya Bashe ni kile kile walichokuwa wanafanya kina Makonda na Jaffo na ndicho anachofanya Majaliwa, kufanya vitu kwa mhemko pale panapokuwa na media. Baada ya kamera kuzimwa na mihemko inaishia hapo hapo hakuna linalotekelezwa.

Bila ya kamera leo hii lini mwisho umemsikia Jaffo. Wakati kipindi cha JPM ilikuwa kila kona yeye. Inamaanisha huu ukimya wake ndio utendaji wake halisi, yale ya kipindi kile yalikuwa maigizo.

Ukiona kiongozi anapostiwa na ma gum boots kwenye matope elewa pembeni skuna zake zipo ndani ya vx huyo ni msanii na hapo yupo location.

Wengi wao wanatembea na watu wa wardrobe, make up na wanakuwa na script kabisa, kuwa leo nitapaza sauti hivi na nitasema hivi. Clip ikisharushwa na movie linaishia hapo hapo.

Bashe ni Kanumba aliyekuwa wizarani. Ni actor.
 
Back
Top Bottom