Ukionewa ni sahihi kushika bunduki na kuingia mtaani kuua watu?

Mi Najua wanaficha ila sababu Ni wAllah hawAkubar
Hawataki kuukubali ukweli. Hamza mwengine atatokea katikati ya mji hatosema anataka police au raia. Atazimimina risasi na mtasema haya maneno tena? Mimi nataka hawa wanaobisha waniletee ushahidi wa hamza akisema amedhulumiwa
 
Katika watu ambao sio shabiki wa matendo ya police na mimi nipo. lakini sijawahi kuwaza kuwaua. acheni ujinga wa kutetea mauaji. Hamza angerusha risasi pale ikampata an innocent person mngesema haya???? Nyie subirini muiskie sababu yake ya kuua ndo mtaelewa. Fuatilieni vitu
 
Kwani wewe unasemaje?
 

Kabisa ,policcm wametengeneza clip ili ionekane hamza ni gaidi,mashuhuda hakuna hata mmoja aliyemsikia akisema hayo maneno....Jamaa kadhulumiwa tu na ma askari.
 
kama hamza angekuwa gaidi basi hao wanne alioua ni wachache sana.pale sarenda kuna kuwa na foleni kuna magari ya kawaida na ya abiria.angeamua kumwaga vyuma pale kuelekezea kwenye magari yale leo tungesema mengine.pia hamza alipishana na watu barabarani wala hakuwa na habari nao.
 
Nimewawekea hadi clip ya hamza. It’s beyond rumours watu wametengeneza story chap ili kufukia adhma ya hamza. He is a killer. Fullstop
Clips huwa zinafanyiwa editing ya kutosha na kuongeza sauti za watu. Kwanza hatuijui hata hiyo sauti ya Hamza inasound vipi.
Na kwa nini clip ilitolewa siku tatu baada ya tukio? Hapa ndiyo utata ulipoanza.
 
Huyu mlinzi binafsi kiherehere alitaka kucheza ngoma sio yke
 
Akikujibu hili kiufasaha nijulishe...
 
Hamza kuua askari kwa hoja ya kudhulumiwa hakumpi haki. Lakini kila tukio lina sababu. Wewe pamoja na wenzio, akiwemo IGP na viongozi wote wa serikali, mnamhukumu Hamza, wakati inadaiwa kuna dhuluma alifanyiwa na polisi na kuwa chanzo cha sakata hili. Mnakwepa kufanya uchunguzi kubaini uhusika wa polisi, ambao si ajabu ndio katj ya hao wanaodaiwa kufa kishujaa na kupewa maziko ya kijeshi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na yote yaliyotokea ambayo sio halali, lakini ukweli ni kwamba hakuna haki katika jamii yetu, kuanzia serikalini, vyombo vya dola ,mahakama,bunge dini na jamii yote kwa ujumla.

Watu pekee wa kuleta haki ni mahakama lakini matukio ya hivi karibuni yana thibitisha haki haipatikani huko tena.

Police wamekua ni watu wa kati ya jamii na mahakama lakini matokeo yake polisi wametugeuka!

Matokeo yake ni haya ya ndugu hamza na watu wengi kuwa upande wa hamza kwa sababu wengi wetu tumekuwa waathirika kwa namna moja ama nyingine na polisi.

Kinachopaswa polisi wajisahihishe kwa kweli, ama kuwe na mjadala wa kitaifa namna polisi watakavyo fanya imani kwa jamii na utumishi wao kwa jamii uthaminike tena.


Pole kwa wote walio athirika, pole kwa familia ya hamza, pole kwa familia ya ndugu polisi waliopoteza maisha, na taifa kwa ujumla.

Lakini igp umeweza kukosea tena, jisahihishe, polisi kwa ujumla wote nanyi mjisahihishe.

Jana ilikuwa bora kadhalika na na leo lakini kesho ni bora zaidi, ila kesho bora huandaliwa na leo.
Jisahihisheni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa technolojia ya leo usiamini video hizo 100%, (unless ur among them) Zinaweza kuwa fake! Hata za kuonesha Hamza akimchinja polisi zinaweza tengenezwa. Kumbuka mapanga, mashoka, visu, pinde na mishale vilivyo kuwa vikioneshwa kwamba vimeagizwa toka nje na CUF enzi hizo.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Simuhukumu kwa kusoma Misri; ila inaonekana kuna mambo alijifunza huko; ambayo yanamtofautisha na raia/mwananchi wa kawaida. Moja wapo ni lile la kutumia silaha nzito kama zile; hakuna mafunzo kama yale yanayofundishwa kwa raia wa kawaida. Tena alikuwa anazitumia kwa ufanisi wa kulenga target kwa hali ya juu sana. Hayo mafunzo hayatolewi kwa raia wa kawaida. Pia kuwa na ile roho (sipirit) ya kuua. Binadamu wa kawaida ni ngumu kuwa na hiyo spirit; tena ukichukulia alianza tu from no where; na kuua polisi wawili; na kuchukua silaha zao. Hivyo vitu ndio vinaashiria kuna kitu alikuwa nacho zaidi ya raia/mwananchi wa kawaida. Huyo alipata training ya kufanya hivyo. Kibaya zaidi ni kuwa kwa umri wake; yeye hakuwahi hata kupitia JKT - maana wakati wao kulikuwa hakuna hayo mafunzo. Hivyo kuna sehemu amejifunza binafsi. Sasa tujiulize; alijifunza akiwa na lengo gani?
 
Kamanda Siro anawaasa wazazi wasizae au kulea watoto wakorofi, na waharifu. Anasahau kuwa jeshi lake ndio linaharibu watoto wa watu. Polisi wanalalamikiwa kutenda maovu mengi, tabia hiyo wamefunzwa huko polisi kwani kabla ya kuajiriwa huchujwa ngazi tofauti tofauti kuanzia mtaani. Au si watu, bali ni robot wametengenezwa kiwanda cha polisi?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…