Pamoja na yote yaliyotokea ambayo sio halali, lakini ukweli ni kwamba hakuna haki katika jamii yetu, kuanzia serikalini, vyombo vya dola ,mahakama,bunge dini na jamii yote kwa ujumla.
Watu pekee wa kuleta haki ni mahakama lakini matukio ya hivi karibuni yana thibitisha haki haipatikani huko tena.
Police wamekua ni watu wa kati ya jamii na mahakama lakini matokeo yake polisi wametugeuka!
Matokeo yake ni haya ya ndugu hamza na watu wengi kuwa upande wa hamza kwa sababu wengi wetu tumekuwa waathirika kwa namna moja ama nyingine na polisi.
Kinachopaswa polisi wajisahihishe kwa kweli, ama kuwe na mjadala wa kitaifa namna polisi watakavyo fanya imani kwa jamii na utumishi wao kwa jamii uthaminike tena.
Pole kwa wote walio athirika, pole kwa familia ya hamza, pole kwa familia ya ndugu polisi waliopoteza maisha, na taifa kwa ujumla.
Lakini igp umeweza kukosea tena, jisahihishe, polisi kwa ujumla wote nanyi mjisahihishe.
Jana ilikuwa bora kadhalika na na leo lakini kesho ni bora zaidi, ila kesho bora huandaliwa na leo.
Jisahihisheni.
Sent using
Jamii Forums mobile app