Nimefuatila ibada mbashara ya kumuweka wakfu Ask. Robert Pangani wa kanisa la Moravian Jimbo la kusini Magharibi - Mbeya ambapo mgeni rasmi ni Mhe. Rais Dr. Samia ambaye amewakirishwa na Naibu Waziri Mkuu. Mkuu huyu wa mkoa ni mweupe kanisa, hajui itifaki, kwanza amepewa nafasi kumkaribisha mgeni rasmi, yeye pamoja na kuwatambulisha wageni alioambatana nao ndani ya mkoa alianza kutoa hotuba yake na ametumia muda mrefu karibu sawa na aliotumia mgeni rasmi,. Pili hajui maana ya kumtuma au kumpatia ruhusa kiongozi aliyechini yake. Katika maelezo yake anadai amemtuma Mkuu wa wilaya mmoja ambaye hakuwepo kwenda kuvishwa nishani ya kijeshi kwani ni mwanajeshi. Kazi anayoifanya makonda kusikiliza malalamiko ya wananchi ambayo yaliyo mengi yanahitaji uelewa wa sheria Mkuu wa mkoa kama Homera asingeyaweza. Na wengi wangeona ukuu wa mkoa au wilaya ni mgumu sana. Na wananchi wangeona umuhimu wa vyeo hivi Kwa Sasa.