Ukipanda Basi unafika Dar mapema kuliko aliekata tiketi ya ndege za ATCL

Ukipanda Basi unafika Dar mapema kuliko aliekata tiketi ya ndege za ATCL

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Iwe unatokea Mbeya au Mwanza ukipanda basi lolote lile hata iwe luwinzo mbona unaweza kufika mapema kuliko aliyekata tiketi ya ndege za ATCL.

Au mmoja akitoka Mwanza akifika Tinde akapanda tank la mafuta mbona unatangulia kufika yaani wewe wa basi unaenda kumpokea mtu aliyepanda ndege.

Ukipanda basi unafika, unakula halafu unapanda daladala kwenda airport kumpokea mtu mliyeachana yeye anaenda airport wewe unaenda Uyole kutafuta basi au Nyegezi, maana wanakalishwa masaa hadi kumi ninyi mnakua mbali yaani mnachapa mwendo kuliko wao kama hamuamini mje kujaribu muone inakuaje.
 
Aisee ukitaka kuharibu programe zako panda ATCL.

Ndege imebalishwa time mara 2 nikamuuliza mtoa huduma wa Aiport ananimbia hilo ni tatizo sugu la ATCL eti ndege zipo chache nyingine zipo busy na viongozi 🤣🤣🤣

Kuanzia sasa nitapanda Precsion hata kama ina makelele kama jenereta.
 
Iwe unatokea mbeya au mwanza ukipanda basi lolote lile hata iwe luwinzo mbona unaweza kufika mapema kuliko aliekata tiketi ya ndege za ATCL.
Au mmoja akitoka mwanza akifika tinde akapanda tank la mafuta mbona unatangulia kufika yaani wewe wa basi unaenda kumpokea mtu aliepanda ndege.
Ukipanda basi unafika, unakula halafu unapanda daladala kwenda airport kumpokea mtu mlieachana yeye anaenda airport wewe unaenda uyole kutafuta basi au nyegezi, maana wanakalishwa masaa hadi kumi ninyi mnakua mbali yaani mnachapa mwendo kuliko wao kama hamuamini mje kujaribu muone inakuaje.
Hapana huu ni uongo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni trip moja iliyochelewa, usijumuishe trip zote
Sio trip moja, mimi go and return zote zimechelewa na nikaambiwa na mtoa huduma wa hapo aiport kuwa ATCL ina tatizo sugu la uchelewaji.

Last week walichelewa zaidi ya saa 5 eti wakawapa abiria offer ya popcorn kuwafuta machozi, wazungu wakatukana sana na kumwaga hizo popcorn.
 
Fast Jet ilikua mkombozi wetu nayo ikafanyiwa hujuma ili ATCL asiwe na mpinzani.
Waswahili wanasema "usijisifu una mbio msifu anayekufukuza" yaani uwepo wa Fast Jet ungewafanya ATCL wasilale wapambane kuboresha huduma kwa weledi na ufanisi Sasa wamemuua mpinzani wao kwa akili mbovu za wivu na roho mbaya ya mwendazake aliyecopy thesis ya Phd
kwanza serikali kununua mindenge ambayo hawawezi kuziendesha ni bora wangeweka mazingira mazuri kwa wazawa kuwekeza huko wao kipaombele ingekua huduma muhimu kwa wananchi saa ivi tusingekua tunapigwa kwenye tozo na Kodi za mafuta,miamalana luku
 
Haya tulipaswa kuyaelewa miaka 50 iliyopita sasa tunayajua leo baada ya kukubali kuiua fastjet, roho ngumu Precision na wengine ili tubakiwe na shirika moja tu likidhani litapata pesa yote. Waulizeni hata Emirates au KQ management zao sio za kugawiana vyeo bali wanwaweka watu competent hata kama sio Waarabu wenzao mradi shirika liende vizuri tu.
Hapa hadi uwe mwenzao au uwe na kadi ya chama na business plan anakaa nayo mtu mfukoni
 
Waswahili wanasema "usijisifu una mbio msifu anayekufukuza" yaani uwepo wa Fast Jet ungewafanya ATCL wasilale wapambane kuboresha huduma kwa weledi na ufanisi Sasa wamemuua mpinzani wao kwa akili mbovu za wivu na roho mbaya ya mwendazake aliyecopy thesis ya Phd
kwanza serikali kununua mindenge ambayo hawawezi kuziendesha ni bora wangeweka mazingira mazuri kwa wazawa kuwekeza huko wao kipaombele ingekua huduma muhimu kwa wananchi saa ivi tusingekua tunapigwa kwenye tozo na Kodi za mafuta,miamalana luku
Na siajabu ATCL wangejifunza mawili matatu kutoka Fast Jet. Ingewezekana kachero wa TISS angetafutiwa ajira Fast Jet kuwaibia maujanja. Makachero wetu wako busy kuwasulubu wana Chadema.
 
Waswahili wanasema "usijisifu una mbio msifu anayekufukuza" yaani uwepo wa Fast Jet ungewafanya ATCL wasilale wapambane kuboresha huduma kwa weledi na ufanisi Sasa wamemuua mpinzani wao kwa akili mbovu za wivu na roho mbaya ya mwendazake aliyecopy thesis ya Phd
kwanza serikali kununua mindenge ambayo hawawezi kuziendesha ni bora wangeweka mazingira mazuri kwa wazawa kuwekeza huko wao kipaombele ingekua huduma muhimu kwa wananchi saa ivi tusingekua tunapigwa kwenye tozo na Kodi za mafuta,miamalana luku
Lakini si ipo precision air. Au?
 
Back
Top Bottom