Presicion wana kabei nafuu ukilinganisha na mwingine. Arafu Kuna kampuni moja hv nilipanda mwanza Dar. Inakitivii kimoja ndan yaan utafikiria bus au Pengine Bora ya bus. Na hiyo tuliambiwa ndio ndege ya kisasa
View attachment 1900629
Mkuu vipi mliwekewa comedy za mkojan mkaburudika au ilikuaje?
Hapa ndipo nilipoamini hii nchi haina viongozi...Fast Jet ilikua mkombozi wetu nayo ikafanyiwa hujuma ili ATCL asiwe na mpinzani.
Unajua ukitaka kujua hii nchi hakuna planners ni pale ambapo leo hii karne ya 21 na kujigamba kwamba mabarabara mengi kwa sasa ni lami lakini eti Mabus hayaruhusiwi kusafiri usiku!!! Ukiwauliza sababu lijitu linasimama kwenye TV na kudai eti ni kwa sababu za kiu salama, ukiuliza hawa mapolisi wanaokimbizana na CHADEMA mpaka Makanisani na kuwavamia mahotelini usiku wa manane kazi yao hasa ni nini??Usifananishe Luwinzo na vitu vya kijinga chali angu
Na siajabu ATCL wangejifunza mawili matatu kutoka Fast Jet. Ingewezekana kachero wa TISS angetafutiwa ajira Fast Jet kuwaibia maujanja. Makachero wetu wako busy kuwasulubu wana Chadema.
Anayeiua ATCL ni huyo mama. Sio mgt ya ATCL.
YaaniFast Jet ilikua mkombozi wetu nayo ikafanyiwa hujuma ili ATCL asiwe na mpinzani.
Hawana mpinzani ndo maanaSio trip moja, mimi go and return zote zimechelewa na nikaambiwa na mtoa huduma wa hapo aiport kuwa ATCL ina tatizo sugu la uchelewaji.
Last week walichelewa zaidi ya saa 5 eti wakawapa abiria offer ya popcorn kuwafuta machozi, wazungu wakatukana sana na kumwaga hizo popcorn.
Iwe unatokea Mbeya au Mwanza ukipanda basi lolote lile hata iwe luwinzo mbona unaweza kufika mapema kuliko aliyekata tiketi ya ndege za ATCL.
Au mmoja akitoka Mwanza akifika Tinde akapanda tank la mafuta mbona unatangulia kufika yaani wewe wa basi unaenda kumpokea mtu aliyepanda ndege.
Ukipanda basi unafika, unakula halafu unapanda daladala kwenda airport kumpokea mtu mliyeachana yeye anaenda airport wewe unaenda Uyole kutafuta basi au Nyegezi, maana wanakalishwa masaa hadi kumi ninyi mnakua mbali yaani mnachapa mwendo kuliko wao kama hamuamini mje kujaribu muone inakuaje.
Hata ambao ndege ilikuwa hatujawahi kuota kupanda, Fast Jet tulipanda.....Mbeya elf 86 kwa wale tulikuwa tunakata week mbili kabla ya safari na kuna wakati niliwahi panda kwa 66 elf tu mpaka Songwe, hao aitisielo na Presisheni MUNGU anawaona.....tumerudi kwenye IT tuFast Jet ilikua mkombozi wetu nayo ikafanyiwa hujuma ili ATCL asiwe na mpinzani.
Hayo masaa 2 unakuwa umefika zenji unakula urojo tuKwenda Zanzibar ukisafiri kwa meli unafika haraka kuliko Ukienda kupanda ndege
Reporting time Ni masaa mawili kabla kwenye ndege wakati ukipanda meli hayo masaa ya waiting time airport aliyepanda meli anakuwa keshajifikia Zanzibar
Na propaganda zikatumika kuwapotosha wasio na ufahamu kwa misemo ya kibaguzi mabeberu,uzalendo...huku kinachosemwa kikiwa viceversa!C.A.G. alionya na kushauri hili shirika ni kansa isiyotibika, ila watu wanadhani mwendawazimu aliyesema siku ina saa 48 anajua zaidi. Kodi zetu zinatumika kuendesha mashirika yasiyo na maana kama haya, ndio maana kila siku yanaibuka matozo ya kipuuzi.
Hahahahaha yaani ingekuwa usafiri wa barabarani tungesema chombo kinasimama kila kituo...The problem is full capacity na sio matengenezo wala idadi ndogo ya ndege bado wanafanya safari kiswahili kwa kujaribu kufanya delaying