Ni ndoto yakila mtu kuwa na mahali ambapo patampatia ujira ambao utaweza kuyamudu maisha yake, mara nyingi tunapozungumzia neno ajira huwa tunazungumzia watu waliopata elimu juu ya jambo fulani inaweza kuwa ni udaktari, Ualimu, Uanajeshi na taaluma nyinginezo ijapo ajira huwa zinalenga watu wa aina zote yaani walio na elimu na wasio na elimu.
Ajira za watu wasio na elimu mara nyingi huwa za muda lakini zawale walio na taaluma huwa ni ajira za muda mrefu mpaka pale umri wao wakustaafu utakapofika.
Ni jambo lisilopingika kuwa kila mtu mwenye taaluma fulani hupenda kama ikitokea bahati ya kupata ajira basi apate ajira katika maeneo ya mjini, Na wengine hudiriki hata kuacha kwenda kuripoti kazini alikopangiwa eti kwa kigezo tu hataki kufanya kazi kijijini na wengine hudiriki hata kusema kuwa kwa elimu aliyonayo hawezi kufanya kazi kijijini, Ukweli ni kwamba kufanya kazi katika maeneo ya vijijini kuna faida nyingi ikiwemo faida zakimaendeleo ya uchumi na kifamilia. Katika chapisho hili ninakwenda kufumbua macho kwa wale wasiojua faida zakufanya kazi kijijini, Zifuatazo ni faida za kuajiriwa vijijini.
Kijijini kuna vyanzo vingi vya fursa kuliko mjini, Kitega uchumi cha kwanza katika nchi yetu ni kilimo na mahali ambako kilimo kinafanyika ni vijijini huwezi ukakuta shamba la hekari kumi mjini isipokuwa kijijini, Hivyo kwa mtu ambae anahitaji kuwa na vyanzo vya mapato tofauti na ajira aliyonayo jambo lakwanza lazima afikirie kuhusu kilimo. Kilimo ni uwekezaji mzuri sana kwa mtu aliyeajiriwa kinaweza kikampatia kipato cha ziada tofauti na ujira unaolipwa.
Kijijini kuna matumizi madogo yafedha, Vitu vingi kijini hupatikana kwa wingi tena kwa bei rahisi na ndio maana wafanyabiashara hutoka mijini na kwenda vijijini kutafuta vitu vya kuuzaa mijini. Kwa mtu mwenye malengo inakuwa ni rahisi sana kuwekeza pesa kwenye mambo ya msingi kwakuwa matumizi ya fedha kijijini yapo chini hivyo kwa mtu anayetegemea maisha yakulipwa mshahara anaweza akawekeza pesa yake katika vitu vingine ambavyo vitampatia fedha ya ziada, Anaweza akawekeza katika kilimo, ufugaji au hata kuwasogezea wanakijiji huduma muhimu kama vile usafiri, maji au hata maduka ambayo kwake vitamuongezea kipato tofauti na mtu ambae ameajiriwa mjini hawezi kufanya vitu hivyo kwakuwa tayari fursa hizo watu wenye pesa wameshazitumia tena kwakuwekeza pesa nyingi.
Kazi ya mtu aliyeajiriwa kijijini matokeo yake huonekana zaidi kuliko mjini, mara nyingi watu wanaoishi vijijini huwa ni walewale hivyo inakuwa ni rahisi kwa mtu ambae amepata ajira kijijini kuwa na uwezo wakumfuata mtu mmoja mmoja na kujua maendeleo yakile anachokifanyia kazi na kukusanya data kwa urahisi kwakuwa watu wake anawajua na anaweza kuwafikia kirahisi tofauti na mjini ambako kila leo watu wanaingia na kutoka, Mfano mwalimu anaweza akamfuata mwanafunzi ambae labda anamuona hana mahudhurio mazuri darasani na akakutana nae kiurahisi au hata akaonana na wazazi wake kiurahisi na kujua changamoto yake, tofauti na mijini ambako watu huishi kama ndege leo wanaishi nyumba hii na kesho nyumba ile hivyo inakuwa vigumu kwa watoa huduma kuigusa kila familia na kupata matokeo mazuri kutoka kwenye kile wanachokifanya.
Mazingira ya vijijini ni mazuri kwa malezi ya watoto, Ni ukweli uliowazi kuwa siku hizi kwenye miji mingi kuna makundi ya watoto ambayo yanajihusisha na masuala yakihalifu mfano panya road, mtoto anaweza akawa mwema nyumbani lakini kumbe anajihusisha na mambo yakihalifu bila mzazi kujua, Hii ni kwa sababu familia nyingi za mijini hazina ushirikiano mzuri tofauti na vijijini ambako familia zinauhusiano mzuri hivyo ni rahisi kutambua mabadiliko ya tabia ya mtoto, Pia hata kwakujisomea kijijini kunampa mtoto wakati mzuri wakujisomea tofauti na mjini ambako muda wote kunakuwa na makelele ya magari, Viwana, miziki na kadhalika.
Vijijini hakuna vishawishi vya matumizi ya fedha, waajiriwa wengi wamekuwa wakitumia pesa zao vibaya pale wanapopata ujira wao na mwisho kujikuta kuwa ujira wao wameutumia kwa muda mchache na mwisho kuishia maisha magumu mpaka pale watakapopata ujira mwingine, Ukipata ajira kijijini itapunguza kuepukana na vishawishi vya marafiki na vishawishi vya kimazingira vitakavyokufanya ushindwe kuutumia vizuri ujira wako, hivyo ukiajiriwa kijijni unaaepukana na vishawishi hivyo vyote na mwishowe ujira wakounaweza ukawekeza katika mambo ya msingi kama vile ujenzi kilimo na hata biashara.
Kuna mazuri mengi yakuyapata pale unapoajiariwa kufanya kazi katika maeneo ya vijijini, Niwape ushauri kwa wale wenye kasumba yakukataa kufanya kazi katika maeneo ya vijijini kuwa siku zote madini hupatikana vijijini hivyo mjini ni sehemu yakutumia pesa na wanaotafuta pesa mjini mara nyingi huwa wanazitolea vijijini na mjini huwa kama vivuli tu lakini vyanzo vyao vingi na vyanzo vikuu vya vipato vyao huwa vijijini, na ndio maana kuna mtunzi mmoja wa mashahiri aliwahi kuwatungia watoto wake shahiri linalosema kuwa kama wanataka mali watazipata shambani, Jambo lakujiuliza kwanini hakuwaambia kama wanahitaji mali watazipata mjini ? Jitafakari nachukua hatua na uanze kuamini kwamba ukiajiriwa kijijini basi unapawsa ufurahi.

Upvote
3