Viwanda vya kutengeneza vitu vya kurahisisha maisha ya Kila siku kama mashine za kufua na kuosha vyombo Ili zipatikane kwa gharama nafuu, vitu vya kurahisisha upikaji kwa urahisi vile vya kisasa kwa matumizi ya nyumbani maana chakula ni lazima kwa kila binadamu tatizo sisi bado tunatumia mifumo ya kizamani inayopoteza muda na huduma,
viwanda vya kusindika vyakula kwa ubora Ili Kila chakula kiwe ready to cook, ukinunua nyama iwe imeshakatwa, maharage, mchele uwe umeshachambuliwa Ili kutusaidia muda mwingi utumike kufanya kazi Ili kujiinulia uchumi wa Kila familia, kingine sekita ya media kwaajili ya matangazo ya biashara peke kwa gharama nafuu maana hivyo vitu Ili tununue tutahitaji kutangaziwa,
kwenye viwanda vya kutengeneza vitu ajitahidi sana vipatikane vingi maana sisi niwanunuaji wazuri lakini niwavivu wa kutengeneza maana kutengeneza vitu kunahitaji muda nasisi muda wetu ushaharibiwa kutumika vibaya.