Ukipewa nafasi ya kuwashauri vijana wa kitanzania, ushauri gani ungewapa ushauri kwa manufaa ya jamii inayowazunguka na Taifa pia?

Ukipewa nafasi ya kuwashauri vijana wa kitanzania, ushauri gani ungewapa ushauri kwa manufaa ya jamii inayowazunguka na Taifa pia?

Mipaka gani watoke wakati wananyimwa visa, wanazungushwa mpaka watoe chochote kitu
Yaani kupata visa mpaka uwe na ndugu yako anayefanya kazi uhamiaji.

Wasomi field tu mtu anaombwa rushwa sembuse kazi
Vijana waliochukuliwa kwenda kwenye mradi wa kilimo, wamefika kule wametelekezwa

Tenda nyingi wanapewa watu wa nje vijana watafanya nini?
Basi wameamua kujiajiri bado Tra uchwara mambo wanaleta mengi muda mchache huko BRELA sitaki kuongea sana
Visa na uhamiaji wapi na wapi?
Au unamaanisha Passport
Visa zinatolewa na balozi husika
 
Vijana wenzangu watanzania, hakuna Tuzo ya mfanyaji Ngono Bora, Mabinti hawaishi ukianza huwamalizi, Save hela yako na wekeza Siku hizi Uzee unawahi sana.

Tena ni heri uzee huo uwahi ukukute mzima kuliko ukukute tayari una mikosi ya kila aina, ukimwi na ndugu zao kina gono, mafinyofinyoo nk
 
Naomba tofauti ya visa na passport, mimi sijui
Passport ni hati yakusafiria inayoonyesha uraia wa muhusika na identity yake,

Visa ni ruhusa Permit inayotolewa na nchi husika unayotaka kwenda,Visa ni kuruhusiwa kuingia kwenye nchi iliyokupa hiyo visa,Visa normally issued by authorities of the country to be visited,

Passport bila kua na Visa bado haitoshi kuingia kwenye nchi unayotaka kwenda,

Zipo aina nyingi za Visa,kuna nchi ni free visa,unaingia bila kulipia,kuna nchi unaomba visa kwenye balozi zao nje ya nchi zao,kuna visa unagongewa Airport ukisha fika kwenye nchi husika,aina za visa hutegemea makubaliano baina ya nchi husika.
 
Shukrani!
 
Achana na biashara za mtandaoni
Forex,binary, crypto, NFT aviator, betting etc

Utapoteza hela amani na fursa kibao.
 
Vijana wenzangu watanzania, hakuna Tuzo ya mfanyaji Ngono Bora, Mabinti hawaishi ukianza huwamalizi, Save hela yako na wekeza Siku hizi Uzee unawahi sana.

Tena ni heri uzee huo uwahi ukukute mzima kuliko ukukute tayari una mikosi ya kila aina, ukimwi na ndugu zao kina gono, mafinyofinyoo nk
Kabisa mkuu
 
Mipaka gani watoke wakati wananyimwa passport, wanazungushwa mpaka watoe chochote kitu
Yaani kupata passport mpaka uwe na ndugu yako anayefanya kazi uhamiaji.

Wasomi field tu mtu anaombwa rushwa sembuse kazi
Vijana waliochukuliwa kwenda kwenye mradi wa kilimo, wamefika kule wametelekezwa

Tenda nyingi wanapewa watu wa nje vijana watafanya nini?
Basi wameamua kujiajiri bado Tra uchwara mambo wanaleta mengi muda mchache huko BRELA sitaki kuongea sana
wacheni malalamiko na kujiwekea vikwazo vya kila aina.

Munaona vijana wenzenu wa Ethiopia wanavyohangaika, nyinyi munasubiri kulishwa kwa vijiko.

Pia muache matusi kwenye mitandao, Mungu anawapa laana kwa hayo munayofanya mitandaoni.
 
Kwanza vijana wale ambao hawana kazi
  • waache kukaa vijiweni wajishugurishe hata kwa malipo kidogo, watapata uzoezu, hali ya kujituma na kupata fursa zingne
  • waache kuongea kuhusu jana, juz na wakati uliopita, wawe na malengo na mipango kwaajiri ya maisha ya kesho na yajayo
  • waache kuongea pumba na mambo yasiyo na maana et diamond ana hela kumshinda konde, shishi kaachwa tena nk. Wajikitike ktk utafutaji wa taarifa zenye faida\fursa
-wale kkb, watafute mtaji kwa jasho lao na kujiendeleza

wale vijana waliopo ktk ajira wapunguze anasa na starehe wafanye maendeleo

wale greenguard na red brigade waache uchawa na siasa chafu za kuchafuana
 
Hakuna taifa lililo endelea kwa vijana wake ku base na mambo ya kiroho.

Hebu acheni kutoa mawazo uchwara hapa.

Mifumo mibovu ya nchi ndio ina haribu vijana.
Kwani wewe umenielewaje navyozungumzia nguvu ya kiroho hao wote wachina wahindi na wazungu Wana Imani zao ndio wapo miungu yao wanayoiabudu
 
Okey, kama ningepata nafasi ya kuzungumza na vijana ningewapa ushauri ufuatao:
  1. Jitambue na Jithamini: Kila kijana anapaswa kutambua thamani yake binafsi. Kujithamini ni hatua ya kwanza kuelekea mafanikio. Tambua nguvu zako, udhaifu wako, na jitahidi kuboresha maeneo yote muhimu maishani mwako.​
  2. Elimu ni Muhimu: Wekeza muda na jitihada katika kupata elimu bora. Elimu haimaanishi tu masomo ya darasani, bali pia kujifunza ujuzi mbalimbali ambao unaweza kukusaidia kujitegemea na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.
  3. Jitume na Kuwa na Nidhamu: Mafanikio yanahitaji bidii na nidhamu. Fanya kazi kwa bidii, weka malengo, na hakikisha unayatimiza. Nidhamu binafsi itakusaidia kuzingatia malengo yako na kuepuka vishawishi vinavyoweza kukupoteza.
  4. Jifunze Ujuzi wa Kiuchumi: Katika dunia ya sasa, ni muhimu kuwa na ujuzi wa kiuchumi. Jifunze kuhusu uwekezaji, ujasiriamali, na jinsi ya kusimamia fedha zako. Hii itakusaidia kuwa na maisha bora na pia kuchangia katika uchumi wa taifa.
  5. Kuwa na Maadili na Uadilifu: Maadili na uadilifu ni misingi ya kuwa mwanajamii mzuri. Kuwa mwaminifu, mkweli, na mwenye heshima kwa wengine. Hii itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na kuwa na sifa nzuri katika jamii.
  6. Jitolee kwa Jamii: Kujitolea ni njia nzuri ya kutoa mchango wako kwa jamii. Shiriki katika miradi ya kijamii, saidia wenye uhitaji, na kuwa mfano bora kwa wengine. Kujitolea kutakujengea pia mtandao mzuri wa marafiki na fursa mbalimbali.
  7. Afya ni Mali: Afya ni msingi wa maisha bora. Hakikisha unazingatia lishe bora, mazoezi, na kupumzika vya kutosha. Afya njema itakusaidia kuwa na nguvu na uwezo wa kufanikisha malengo yako.
  8. Epuka Madawa ya Kulevya na Vilevi: Madawa ya kulevya na vilevi ni hatari kwa afya na maendeleo yako. Epuka matumizi ya vitu hivi ili kulinda afya yako na kuepuka matatizo yanayoweza kukuzuia kufikia malengo yako.
Kwa ujumla, vijana wanapaswa kutambua kuwa wao ni msingi wa maendeleo ya taifa. Kila kijana anapaswa kujitahidi kuwa bora zaidi, sio tu kwa manufaa yake binafsi bali pia kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla. Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom